-

.

.

TRAMEPRO

TRAMEPRO

NAIPENDA NCHI YANGU TANZANIA

Wednesday 30 July 2014

KATIBU TUWATA KUZIKWA LEO

NA MWANDISHI WETU, Dar
ALIYEKUWA Katibu Mkuu wa Shiririka la Kusaidia Wazee, Tumaini la Wazee Tanzania, (TUWATA) jijini Mbeya, Dk. David Magogo, anatarajiwa kuzikwa leo katika Makaburi ya Uwanja wa Sababasaba jijini humo.
Dk. Mgogo ambaye pia ni mwasisi wa shirika hilo alifariki dunia juzi saa saba mchana katika Hospitali Teule ya Ifisi, nje kidogo ya Jiji la Mbeya alikokuwa amelazwa kwa matibabu.
Msemaji wa TUWATA, Boniventure Mwalongo, aliliambia Raia Tanzania jana jijini Dar es Salaam kuwa, marehemu kwa muda mrefu alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa moyo na tatizo la mfumo wa upumuaji.
“Hivi karibuni alionekana kama afya yake imetengamaa kwa sababu mimi nilikuwa Mbeya siku mbili zilizopita na nilizungumza naye mara kadhaa, lakini kumbe ndio alikuwa kama anatuaga,” alisema Mwalongo.  
 Mwalongo alisema moja ya mambo ambayo yatawafanya wamkumbuke ni kuasisi shirika hilo kwa ajili ya kuwasaidia wazee jijini Mbeya na mikoa ya jirani.
“Baada ya kustaafu aliamua kuanza jitihada za kuunda chombo cha kuwasaidia wazee na hatimaye alifanikiwa kuunda TUWATA ambayo awali, kabla ya usajili, ilifahamika kama Saidia Wazee. Hili ndilo jambo kubwa ambalo ameliacha na atakumbukwa daima,” alisisitiza.
Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Mbeya, Mwenyekiti wa TUWATA, Lydia Njeni, alisema Dk. Magogo ameacha pengo, huku akisisitiza serikali kutowasahau wazee katika suala la matibabu wanapokumbwa na maradhi.
“Dk. Magogo kwa umri wake alikuwa mzee, kweli aliugua kwa muda mrefu na hadi anafariki dunia, nilikuwa naye kwa karibu sana. Ni kama amefia mikononi mwangu. Tatizo lililoko hapa ni gharama kubwa za matibabu kwa wazee kama sisi.
“Kwa mfano, hata ile juzi baada ya kufariki dunia, tukampeleka katika chumba cha kuhifadhia maiti, tukaambiwa tutoe Sh 40,000. Jamani fedha hizi tunazipata wapi sisi wazee? Naona bado Serikali imetusahau sana wazee,” alisema Lydia.
Mratibu wa asasi zisizo za kiserikali katika Halmashauri ya Jiji la Mbeya, Victor Kabuje, alisema atamkubuka Dk. Magogo kama mtu aliyekuwa na ubunifu wa kipekee na hasa katika suala la kuwasaidia watu.
“Mimi nakumbuka jinsi alivyokuja kwangu na tukashirikiana kuisajili TUWATA, baada ya hapo akanipa uanachama wa heshima. Kila wakati alikuwa mtu wa kuja na mawazo mapya,” alisema Kabuje.
Katika hatua nyingine, mtoto wa marehemu, Joyce Magogo, aliwashukuru watu wote waliotoa michango yao ya hali na mali katika msiba wa baba yake.
Dk. Magogo alizaliwa April 2, 1934 wilayani Korogwe, Tanga. Alikuwa na taaluma ya udaktari wa binadamu. Katika nyakati tofauti alifanya kazi katika hospitali za Bugando Mwanza, Kwimba, Tukuyu, Kyela na Mbeya kabla ya kustaafu mwaka 1992.
Ends. 

MWENYEKITI WA TRAMEPRO BWANA SIMBA ABDULRAHMAN SIMBA AKITOA SALAM ZA PONGEZI KWA MHE. DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KWA KUCHAGULIWA KUWA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SEND EMAIL TO TRAMEPRO

Name

Email *

Message *