-

.

.

TRAMEPRO

TRAMEPRO

NAIPENDA NCHI YANGU TANZANIA

Monday 19 September 2016

TRAMEPRO yaandaa mafunzo kwa watoa Tiba Asili

Shirika la Dawa Asili na Ulinzi wa Mazingira nchini Tanzania – TRAMEPRO, limeandaa mafunzo kwa watoa tiba asili na tiba mbadala kutoka maeneo yote nchini.




Katibu Mkuu wa TRAMEPRO, Bw. Boniventura Ferdinand Mwalongo

Lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa watoa tiba asili na tiba mbadala wanafanya shughuli zao kwa kufuata kanuni, sheria na taratibu ili kundoa misuguano isiyo na lazima baina yao na wasimamizi wa sheria.
Katibu Mkuu wa TRAMEPRO Bw. Boniventura Mwalongo amesema hayo jijini Dar es Salaam na kufafanua kuwa mafunzo hayo yatasaidia kuifanya tiba asili nchini kutolewa katika viwango vinavyokubalika na hivyo kuwapa Watanzania huduma bora za tiba asili.
Kuhusu msadaa kwa waathirika wa tetemeko la ardhi lililoikumba mikoa ya Kanda ya Ziwa; Afisa Uhusiano wa shirika hilo Bw. Alberto Sanga amewataka wadau wa mazingira na Watanzania kwa ujumla kushirikiana na serikali katika kuchangia wahanga wa tukio hilo alilosema kuwa chanzo chake ni cha asili na kwamba hakitokani na sababu za kibinadamu.

Saturday 10 September 2016

TAMKO LA KATIBU MKUU WA TRAMEPRO KUHUSU WATOTO WALIOMALIZA ELIMU YA MSINGI LILILOTOLEWA TAREHE 10/09/2016

TRADITIONAL MEDICINE AND ENVIRONMENTAL PROTECTION
SHIRIKA LA DAWA ASILIA NA ULINZI WA MAZINGIRA




TAMKO LA KATIBU MKUU WA TRAMEPRO KUHUSU WATOTO WALIOMALIZA ELIMU YA MSINGI LILILOTOLEWA TAREHE 10/09/2016

Ndugu Waandishi wa Habari,

Katika jamii yoyote ile duniani watoto wote bila kujali kabila, mila, rangi, utaifa,dini, jinsia, ulemavu, hali ya kiuchumi, ukimbizi au hali yoyote , moja ya haki na urithi pekee wenye thamani kwao ni Elimu. Elimu humfanya mtoto aweze kujitambua na kumpa upeo utakaomuwezesha kukabiliana na changamoto mbalimbali za kimaisha ili aweze kuishi vyema katika maisha yake ya hapa duniani.

Nitumie fursa hii kuwapongeza watoto wote waliomaliza mtihani wa Taifa wa kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka huu wa 2016, PONGEZI SANA! Ni jambo muhimu kama wazazi/ walezi na Taifa kwa ujumla kwani hii ni fursa adimu kwa ustawi na maendeleo ya mtoto na ni miongoni mwa njia ya kutimizwa kwa haki ya msingi ya mtoto ya kuendelezwa ambayo inamjengea mtoto msingi imara wa maisha yake ya baadae.

Ndugu Wanahabari, TRAMEPRO tunaipongeza Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kwani Takwimu zinaonyesha kuwa, wanafunzi 795,761 (wavulana 372,883 sawa na asilimia 46.86 na wasichana 422,878 sawa na asilimia 53.14) wamesajiliwa kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu.

Ni matarajio yetu kuona watoto wote wanapata nafasi ya elimu ya Sekondari kwakuwa Msingi tayari umeshawekwa na Serikali yetu tukufu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wa kutoa na imekusudia kumpa kila mtoto Elimu ya Sekondari bure. Hivyo tusingefurahi mmojawapo kati ya watoto hawa waliomaliza elimu ya msingi akaikosa nafasi hii kwa sababu zinazoweza kuzuilika

Hivyo ningependa kutumia fursa hii pia kuwaasa watoto waliomaliza darasa la saba kutojihusisha na tabia au vitendo vyovyote vinavyo hatarisha afya, usalama na maendeleo yao, kama vile kujihusisha kwenye masuala ya ngono, matumizi ya madawa ya kulevya na vileo katika kipindi hiki cha kusubiri matokeo ya mitihani yao.

 Watoto wetu wa Kike na Kiume wajitambue, na wajue kuwa wao ni hazina ya pekee katika maendeleo ya nchi yetu. Kipindi hiki wakitumie vizuri kwa kuwa waadilifu, waaminifu, wenye bidii na kuzingatia kanuni za nidhamu na tabia njema huku wakijiandaa kwa ajili ya kuendelea na elimu ya Sekondari.


Ndugu waandishi

Pamoja na juhudi nzuri ya serikali ya kuhakikisha elimu inapatikana bure kwa watoto wote kuanzia shule ya msingi hadi sekondari, lakini bado kunawananchi wengi hawajapata elimu nzuri na yakutosha kwa kuhusha elimu na mambo ya ushirikina. Hari hiyo hupelekea kukwamisha maendeleo ya elimu kwa watoto na hasa maeneo ya vijijini
Kwa waganga wachache wasiokuwa waaminifu wasiofuata maadili katika utabibu kuihusisha tiba asili na ushirikina. Hali ambayo huchochea umasikini na kukwamisha maendeleo ya elimu

TRAMEPRO inapenda kuwaasa wazazi, walezi na watoto
kuwaasa watoto wote kutumia kipindi hiki kwa kukataa kurubuniwa, kushawishiwa na kujiingiza katika mambo yenye kuhatarisha afya, usalama na maendeleo yao.

TRAMEPRO inawataka Wazazi Walezi Watoto na jamii kwa ujumla:-

1.  Kuwashirikisha watoto katika shughuri mbalimbali za usafi na ulinzi wa mazingira katika kipindi hiki cha kusubiria matokeo yao na isiwe Kuwaozesha watoto wa wao waliohitimu darasa la saba kwa sababu yoyote ile au kwa lengo la kujipatia mali kwa njia ya mahari.

2.  Kuwashirikisha watoto kupata maoni yao, kujiunga na vikundi mbalimbali vya stadi za maisha, kama michezo  kusikilizwa na kushiriki kwa hiari yake katika maamuzi yahayohusu maisha yake kulingana na umri na upeo wake.

3.  Kuwapa uhuru watoto wa kujifunza asili yao, tamaduni zao kwa kuwaelimisha kutofuata matembo mabaya yanayofanywa na baadhi ya wanajamii kwa mfano kujiepusha na jamii zenye Imani potofu kama unyanyapaa kwa watu wenye ualbino.

4.  Kuwaasa watoto kujiepusha na kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi wakiwa na umri mdogo pamoja na kuwapa elimu juu ya magonjwa ya kuambukiza na mimba katika umri mdogo.  Kwa mujibu wa Sheria ya makosa ya kujamiiana ya mwaka 1998 ambayo imefanyiwa marekebisho na kuhuishwa kwenye Makosa ya Jinai (Penal Code Cap 16)  inaelekeza kuwa ni kosa la jinai  kwa mtu yoyote kumlaghai mtoto wa umri wa chini ya miaka  18 kwa kumpa mimba au kufanya nae mapenzi.

5.  Pia tunapenda kuwaasa watoto kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na kwa wazazi kutotoa fursa kwa watoto kutumia vibaya mitandao ya kijamii

Lengo ni kuona jamii ya watanzania inafikia malengo yake kwa kutokomeza umaskini, ujinga na maradhi kwa kuwatimizia watoto haki ya elimu ili waweze kutimiza ndoto zao na kulijenga taifa letu la Tanzania


Imetolewa na:-

BONIVENTURA F. MWALONGO
KATIBU MKUU WA TRAMEPRO
DAR ES SALAAM

10/09/2016

Thursday 1 September 2016

TRAMEPRO YAUNGANA NA SERIKALI KATIKA MAADHIMISHO YA TIBA ASILI YA MWAFRIKA KWA NCHI 46 ZA AFRIKA - WHO-AFRO

Shirika la Dawa Asilia na ulinzi wa mazingira TRAMEPRO. Tanzania Bara TUNAUNGANA NA SERIKALI,KATIKA NCHI 46 BARANI AFRIKA KUADHIMISHA SIKU YA TIBA ASILI YA MWAFRIKA Tarehe 31/08/2016.Bara la Africa WHO-AFRO.UJUMBE Maalum wa mwaka huu ni "Kanuni za udhibiti wa bidhaa za Tiba Asili Katika Kanda ya Afrika" Mganga wa Tiba Asili zingatia Sera,Sheria,Kanuni ,Taratibu na Miongozo inayo simamia huduma ya Tiba Asili.TAMKO LA KATIBU MKUU KUHUSU MAADHIMIMISHO YA SIKU YA TIBA ASILI YA MWAFRIKA lililotolewa 31/08/2016.KATIKA UKUMBI WA WAZIRI WA AFYA MAENDELEO YA JAMII ,JINSIA ,WAZEE NA WATOTO.
picha ni kumbukumbu mbalimbali za maonesho ya Tiba asili ya Mwafrika yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam - TANZANIA Mnamo mwaka 2014.




MWENYEKITI WA TRAMEPRO BWANA SIMBA ABDULRAHMAN SIMBA AKITOA SALAM ZA PONGEZI KWA MHE. DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KWA KUCHAGULIWA KUWA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SEND EMAIL TO TRAMEPRO

Name

Email *

Message *