-

.

.

TRAMEPRO

TRAMEPRO

NAIPENDA NCHI YANGU TANZANIA

Sunday 4 December 2016

TAARIFA YA MHE. UMMY MWALIMU (MB); WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KWENYE UZINDUZI WA VYETI NA MIHURI MIPYA YA CHANJO YA UGONJWA WA HOMA YA MANJANO 24 NOVEMBA, 2016

Ugonjwa wa Homa ya Manjano husababishwa na virusi ambavyo huenezwa na mbu aina ya `Aedes` ambaye huweza kuvichukua virusi kutoka kwa wanyama aina ya nyani au kutoka kwa mtu mwenye ugonjwa huu na kuambukiza mtu mwingine kwa kumuuma.

Image result for ummy mwalimuPamoja na kueneza virusi vinavyosababisha Homa ya Manjano (Yellow Fever), mbu huyu pia huweza kueneza virusi vinavyosababisha Homa ya Zika, Homa ya Dengue na Chikungunya. Hivyo udhibiti wa Mbu huyu aina ya Aedes unachangia sana katika kudhibiti magonjwa haya kwa pamoja.

Ndugu Wananchi,
Dalili za mtu mwenye ugonjwa wa Homa ya Manjano ni pamoja na kuwa na homa, kuumwa na kichwa, maumivu ya misuli pamoja na mgongo, mwili kutetemeka, kupoteza hamu ya kula, kusikia kichefuchefu,  kutapika na mwili kuwa na rangi ya manjano.

Dalili nyingine ni kutokwa na damu sehemu za wazi kama mdomoni, puani, machoni na masikioni. Pia wakati mwingine damu huonekana kwenye matapishi, kinyesi na figo kushindwa kufanya kazi. Kipindi cha kuonekana kwa dalili za ugonjwa huu ni kati ya siku 3 hadi 6 baada ya kuambukizwa.

Ndugu Wananchi,
Ugonjwa wa Homa ya Manjano hauna tiba kamili na hivyo mtu akiupata anaweza kupoteza maisha kama hajapata huduma za afya mapema. Hata hivyo, ugonjwa huu una chanjo ambayo mtu akipata humkinga asipate maambukizi. Chanjo hii imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa na uwezo wa kukinga mtu dhidi ya maambukizi ya virusi kwa kipindi chote cha maisha yake. Hii ina maana kuwa hivi sasa mtu akipata chanjo hiyo mara moja itatosha kumkinga kwa maisha yake yote.

Ndugu Wananchi,
Kama mnakumbuka tarehe 21 Machi 2016 nilitoa tamko la tahadhari ya ugonjwa wa Homa ya Manjano kutokana na taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa huu katika nchi jirani ya Kenya, Angola na DRC.

Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Afya Duniani hadi kufikia mwezi Oktoba, 2016 tokea mlipuko ulipoanza mwezi Desemba, 2015 imeripotiwa kuwa idadi ya wagonjwa wa homa ya manjano katika nchi ya Angola ni takribani watu 4,347 na zaidi ya watu 377 walipoteza maisha. Hali kadhalika, katika nchi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo idadi ya wagonjwa ilikuwa 2,987 na zaidi ya watu 121 walipoteza maisha. Takwimu hizi zinaonesha jinsi gani ugonjwa huu ulivyokuwa hatari na jinsi unavyoweza kusambaa kwenye nchi zingine. Habari njema, Tanzania haijawahi kuripoti kuwa na mgonjwa wa Homa ya Manjano toka mwaka 1960.

Ndugu Wananchi,
Kila mtu yupo kwenye hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa Homa ya Manjano, ila makundi yafuatayo yapo katika hatari zaidi ya kupata ugonjwa huu;
·        Wasafiri ambao hawajapata chanjo na wanaotembelea nchi ambazo tayari zina maambukizi ya ugonjwa wa Homa ya Manjano.
·        Watu wanaojihusisha na shughuli za uwindaji, utalii n,k.
·        Wafanyakazi wa Viwanja vya Ndege, Bandari na mipaka ya nchi kavu.

Wizara yangu inaratibu utoaji wa Chanjo ya Homa ya Manjano kupitia vituo vilivyoidhinishwa hapa nchini kwa mujibu wa Kanuni za Afya za Kimataifa, 2005 na Sheria ya Afya ya Jamii, 2009. Mtu anapopata chanjo hii hupewa cheti maalumu cha chanjo ya Homa ya Manjano yaani ‘International Certificate of Vaccination and Prophylaxis’ kama utambulisho kwamba, tayari amepata chanjo ya Homa ya Manjano.

Hata hivyo, Utoaji wa Chanjo hiyo umekuwa ukikabiliwa na changamoto ya kuwepo kwa baadhi ya wananchi wasiokuwa waaminifu maarufu kama ‘vishoka’ ambao wanagushi vyeti vya chanjo na kuwapatia wasafiri pasipo kuchanja. Taarifa za kugushi vyeti ziliripotiwa hata na gazeti la ‘The Citizen’ la tarehe 7 Juni, 2016 na vyombo vingine vya habari ambavyo vilibainisha uwepo wa vishoka hao nje ya hospitali ya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam ambao huwalaghai wasafiri na kuwauzia vyeti pasipo kupewa chanjo. Hii ni kinyume na Sheria ya Afya Jamii ya Mwaka, 2009.

Ndugu Wananchi,
Kutokana na mabadiliko ya teknolojia, vyeti vya zamani vimekuwa rahisi kutengenezwa na watu na kutolewa bila kupata chanjo, Hivyo Wizara imefanya maboresho ya vyeti vya chanjo ya Homa ya Manjano kwa kuweka alama za siri na kutengeneza mihuri mipya. Vyeti hivi sasa vina kurasa 16, (vya zamani vina kurasa 8) namba ya utambulisho (serial number) na vinatolewa na vituo vilivyoidhinishwa na Wizara. Aidha vyeti hivi vitaendana na kuweka namba ya utambulisho wa chanjo (Batch number) iliyotolewa ili kuepusha tabia ya watumishi wasiokuwa waaminifu kuvitoa bila kuchanja. Vyeti hivi nitavizindua hivi punde.

Ndugu Wananchi,
Ubadilishaji wa vyeti vya chanjo utafanyika katika awamu mbili kama ifuatavyo;

Awamu ya kwanza; ilihusisha utoaji wa vyeti vipya kwa wanaochanja kuanzia tarehe 1 Agosti, 2016 na kuendelea. Gharama za Huduma za Chanjo ya Homa ya Manjano ni shilingi elfu 20 za Kitanzania kwa raia wa Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa raia wa Kigeni ni Dola 50 za Kimarekani.

Awamu ya pili; itajumuisha ubadilishaji wa vyeti vya zamani kwa wale ambao walipatiwa chanjo na kupewa vyeti halali vya zamani. Wahusika wa kundi hili watawasilisha vyeti vya vya zamani kwa Mganga Mkuu wa Mkoa/Wilaya wa sehemu waliyopo ambaye atawasilisha taarifa zao Wizarani ambapo zitahakikiwa na wale wanaostahili watatumiwa vyeti vyao mahali walipo.  Zoezi hili litadumu kwa takribani miezi mitatu kuanzia  tarehe 09 Januari, 2017 mpaka Machi 31, 2017. Napenda kuwajulisha kuwa kuanzia tarehe 01 Aprili, 2017 vyeti vya zamani havitatambulika tena.

Ndugu Wananchi,
Ninawaagiza Maafisa Wafawidhi wa Vituo vilivyoidhinishwa na Wizara kwa ajili ya kutoa Chanjo ya Homa ya Manjano kuzingatia yafuatayo;
1.   Kuhakikisha vyeti vya chanjo vinatolewa mara baada ya mtu kukamilisha malipo na kupewa chanjo na si vinginevyo. Wizara  itawachukulia hatua wale wote watakaotoa vyeti bila kutoa chanjo.
2.   Kuhakikisha chanjo inatolewa pale tu ambapo malipo yamefanyika na kuna risiti halali ya malipo.
3.   Kuzingatia maelekezo ya utunzaji wa fedha, ujazaji sahihi wa vyeti na utunzaji wa kumbukumbu za waliopata chanjo.
4.   Kuwasilisha taarifa za waliopata chanjo na vyeti vya chanjo kila mwezi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto.

Ndugu Wananchi,
Napenda kuwafahamisha kuwa ugonjwa wa Homa ya Manjano bado haujaingia nchini. Hivyo, ninawasihi wananchi wote na wasafiri tushirikiane katika kudhibiti ugonjwa huu usiingie nchini mwetu kwa kuzingatia yafuatayo:-
1.   Kuepuka kupokea au kununua vyeti bila kupata chanjo kwani kufanya hivyo kunahatarisha maisha yako na ya watu wengine. Aidha, toa taarifa kwenye ofisi yoyote ya serikali iliyo karibu au vyombo vya dola juu ya Afisa au mtu anayetoa cheti bila kutoa chanjo au mtu anayetoa chanjo bila kutoa risiti.
2.   Iwapo unasafiri, kuhakikisha unapata chanjo siku 10 kabla ya kusafiri na kisha kupewa cheti cha kuthibitisha kupata chanjo hiyo pamoja na stakabadhi ya Serikali baada ya kukamilisha malipo. Ifahamike kuwa chanjo ya Homa ya Manjano inatolewa katika vituo vifuatavyo;

a.   Viwanja vya Ndege
Uwanja wa Ndege wa Kimaitaifa wa Julius Nyerere, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro na Uwanja wa Ndege wa Mwanza.

b.   Bandarini
Bandari ya Dar es Salaam, Bandari ya Tanga, Bandari ya Mwanza, na Bandari ya Kigoma.

c.   Mipaka ya nchi kavu
Horohoro, Namanga, Holili, Tarakea, Sirari, Isaka, Mutukula, Mtambaswala, Kasumulu na Tunduma.

d.    Dar e s salaam
Kituo cha Afya cha Mnazi Mmoja.

3.   Wizara inatoa onyo kwa vituo vinavyotoa chanjo bila kuwa na kibali kuacha mara moja. Hali kadhalika wale wanaochapisha, kusambaza na kuuza vyeti hivi waache mara moja kwani hatua kali itachukuliwa dhidi yao.

Hitimisho:
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inapenda kusisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kuchukua tahadhari ya Ugonjwa wa Homa ya Manjano hususani wale waliopo katika mikoa ambayo inapakana na nchi ya Uganda, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo pamoja na maeneo yote ambayo watu hupita kuingia nchini kwenye mipaka ya nchi kavu, maziwa, viwanja vya ndege na bandari. Ninawashukuru na ninawaomba tusaidiane katika kuimarisha udhibiti wa Ugonjwa huu usiingie hapa nchini. Mwisho, napenda kuchukua nafasi hii kuwashukuru Shirika la Afya Duniani (WHO) na Wadau wengine wa Maendeleo kwa jitihada zao za kuboresha udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza yenye hatari ya kusambaa Kimataifa. Asanteni sana.

Baada ya kusema hayo natangaza rasmi kuwa vyeti vipya vya Chanjo ya Homa ya Manjano yaani International Certificate of Vaccination and Prophlaxis ambavyo vinatolewa kwa mujibu wa Kanuni za Afya za Kimataifa, 2005 na Sheria ya Afya ya Jamii, 2009 vimezinduliwa rasmi.

ASANTENI SANA KWA KUNISIKILIZA.

TAARIFA YA MHE. UMMY MWALIMU (MB); WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO KWENYE UZINDUZI WA VYETI NA MIHURI MIPYA YA CHANJO YA UGONJWA WA HOMA YA MANJANO 24 Novemba, 2016

Ndugu Wananchi,
Ugonjwa wa Homa ya Manjano husababishwa na virusi ambavyo huenezwa na mbu aina ya `Aedes` ambaye huweza kuvichukua virusi kutoka kwa wanyama aina ya nyani au kutoka kwa mtu mwenye ugonjwa huu na kuambukiza mtu mwingine kwa kumuuma.

Pamoja na kueneza virusi vinavyosababisha Homa ya Manjano (Yellow Fever), mbu huyu pia huweza kueneza virusi vinavyosababisha Homa ya Zika, Homa ya Dengue na Chikungunya. Hivyo udhibiti wa Mbu huyu aina ya Aedes unachangia sana katika kudhibiti magonjwa haya kwa pamoja.

TAMKO LA MHESHIMIWA UMMY A. MWALIMU (MB), WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO WAKATI WA UZINDUZI WA FOMU YA USAJILI WA DAWA ZA TIBA ASILI, KUNDI LA PILI

Image result for ummy mwalimu
Kama mnavyofahamu, Serikali inatambua umuhimu wa Tiba Asili ambayo ni tiba kongwe zaidi nchini, imekuwepo toka enzi na enzi. Pia, watanzania zaidi ya asilimia sitini (60%) wanatumia huduma hii ya Tiba Asili. Hivyo, ni muhimu kuhakikisha kuwa inaboreshwa na kuendelezwa ili kupanua wigo wa watumiaji, huku tukiwa na uhakika wa ubora na usalama wa huduma hii. Katika kutekeleza hayo, Serikali imerasimisha Tiba Asilia kwa kujumuisha Tiba Asili na tiba Mbadala kwenye Sera ya Afya pamoja na kutunga Sheria.

Ndugu Wananchi,
Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala lilianzishwa kisheria chini ya Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala Na.23 ya Mwaka 2002, kwa lengo la kusimamia, kudhibiti na kuendeleza huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini. Baraza lilizinduliwa rasmi mwaka 2005.

Usajili wa Waganga wa Tiba Asili na Tiba Mbadala, Wasaidizi na vituo vya kutolea huduma ulianza rasmi mwaka 2011. Hadi sasa Baraza limefanikiwa kusajili waganga zaidi ya elfu kumi na nne (14,000) na vituo mia moja na themanini (180).

Ndugu Wananchi,
Pamoja na mafanikio hayo, Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za Serikali limeweka mfumo unaoweza kuwasaidia walaji kuhakikisha kuwa wanatumia dawa za asili zilizo salama kwa kuzipima katika maabara zinazotambulika na Serikali. Dawa zitakazopimwa zitawawezesha waganga kusajili dawa zao, na hivyo kuwasaidia kufanya kazi kwa kujiamini na kupata soko ndani na nje ya nchi na kuongeza kipato chao binafsi na kwa Taifa.

Ndugu Wananchi,
Usajili wa dawa za tiba asili utategemea vigezo vifuatavyo:
·        Mtaalamu wa tiba asili lazima awe amesajiliwa kisheria na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala na ana leseni ya kufanyia kazi iliyo hai.
·        Kituo cha kutolea huduma lazima kiwe kimesajiliwa na kina leseni iliyo hai. Sehemu ya kuzalishia dawa iwe imekaguliwa na kuthibitika kuwa inafaa kwa kuzalishia dawa.
·        Mtaalamu wa tiba asili anapaswa kuwasilisha katika Ofisi ya Msajili wa Tiba Asili na Tiba Mbadala, taarifa sahihi za uchunguzi wa dawa yake kutoka katika taasisi zilizoainishwa katika fomu ya usajili wa dawa. Taasisi hizo ni BRELA, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Mabaara ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Taasisi ya Chakula na Lishe, Maabara ya Taifa ya Afya, Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu.

Serikali linawaasa waganga wa tiba asili na tiba mbadala wote kufuata sheria na kuhakikisha kuwa dawa zinaandaliwa kwa ubora na zinasajiliwa kwa mujibu wa sheria ili kuinua tiba asili nchini. Naliagiza Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kusimamia suala hili kikamilifu.

Kwa kusema hayo nazindua rasmi usajili wa dawa za tiba asili leo tarehe 24/11/2016.

Ahsanteni kwa kunisikiliza. 

MWENYEKITI WA TRAMEPRO BWANA SIMBA ABDULRAHMAN SIMBA AKITOA SALAM ZA PONGEZI KWA MHE. DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KWA KUCHAGULIWA KUWA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SEND EMAIL TO TRAMEPRO

Name

Email *

Message *