-

.

.

TRAMEPRO

TRAMEPRO

NAIPENDA NCHI YANGU TANZANIA

Tuesday 23 August 2016

TIBA ASILIA NA TIBA MBADALA TANZANIA NA SHIRIKA LA DAWA ASILIA NA ULINZI WA MAZINGIRA TANZANIA (TRAMEPRO)

TRAMEPRO ni Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira (Traditional Medicine and Environmental Protection Organization) lililosajiliwa chini ya Sheria ya Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali yaani Non – Govermental Organization (NGO’s) “Act 24 of 2002” lenye namba ya usajili 00NGO/00007772 linalofanya kazi kwa Karibu na Serikali na Jamii katika kufuatilia Matumizi sahihi ya dawa asilia , uandaaji wa dawa asilia, upatikanaji wa dawa asilia na uvunaji endelevu utakao pelekea kukua kwa pato la mtu mmoja mmoja na uchumi wa nchi pamoja na kulinda Mazingira ili kupata dawa asili iliyo na Virutubisho vya kutosha . Uvunaji makini wa Miti dawa utatuletea upatikanaji wa mvua za kutosha zitakazo tuwezesha katika kilimo, hewa safi, chakula pia kulinda na kuendeleza BAONUAI.
Image result for tiba asiliDira ni kuwa na Jamii yenye kuheshimu, kutumia na kulinda Dawa za Asilia zinazotoka katika mazingira Asili na yaliyolindwa, ili kutuwezesha kuwa na Afya bora, kupambana na adui maradhi nakutambua vyanzo vinavyoweza kuchafua matumizi yetu Salama na kulinda usalama wa watumiaji.
Kwapamoja tunawajibu mbalimbali katika kuangalia upatikanaji na upandaji wa miti dawa ili kupata dawa kwa wingi na kuendelea kulinda Afya zetu na kutunza mazingira yetu. TRAMEPRO tunafanya juhudi mbalimbali za kuhakikisha jamii inapata elimu ya matumizi ya dawa asili na faida zinazopatikana kwa kulinda mazingira yetu .Ili kufanikisha matumizi sahihi ya Dawa asilia na kulinda Mazingira ni muhimu Kutoa Elimu na kuwajengea uwezo waganga, watabibu, wavunaji, wakulima, wazalishaji, wauzaji na Watumiaji wa dawa asilia.
Image result for tiba asiliTRAMEPRO kupitia semina, midaharo, makongamano mbalimbali tuliyoandaa na kushirikishwa (kushiriki), vipindi katika redio na television pamoja na mitandao yetu ya kijamii tumejitahidi kuelimisha matumizi sahihi ya dawa asilia na utoaji wa huduma sahihi za tiba asilia kwa matabibu kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyowekwa ili kuhakikisha kuwa jamii inakuwa na uelewa mkubwa juu ya matumizi sahihi ya dawa asili na kulinda mazingira yetu.             
Kwa kutambua Sera, Sheria, Kanuni, taratibu na miongozo inayo simamia shughuri zetu za kila siku na kushirikiana na wadau wa afya na Mazingira  hasa katika kufanya utafiti wa Dutu za mimea,wanyama, madini, ndege na wadudu tutakuza sekta yetu ya Tiba Asilia na Tiba Mbadala.
Leo tumekutana hapa na wadau mbalimbali wa Afya, Tiba Asilia, Tiba Mbadala na mazingira ili kujadili maelekezo na utekelezaji wa Maagizo ya Serikali ya tarehe 15 Januari 2016 yaliyotolewa na Mhe. Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kwa watabibu wa Tiba Asili na Tiba Mbadala, kubadilishana uzoefu, ujuzi na maarifa kati yetu na wadu wengine juu ya njia bora na sahihi za kuwahudumia wagonjwa, ili kupunguza madhara yatokanayo na uzembe, ucheleweshaji na matukio mengine yanayoweza kusababisha ulemavu na vifo.
Pia kutoa elimu nasaha juu ya afya ya msingi kwa wateja wao, na kuleta uhusiano mzuri na wakaribu kwa wote, ikiwa ni pamoja na watabibu wa Tiba Asilia na Tiba Mbadala na jamii yote tukiwa na matarajio ya kuongeza upeo zaidi.
Shirika la dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira TRAMEPRO linaungana katika Mkutano huu ikiwa ni moja kati ya mikutano iliyoshiriki na kuandaa ili kupata maoni ya wadau  na kuongeza upeo zaidi juu ya huduma za Afya zinazotolewa kwa Tiba Asilia na tiba Mbadala na namna ambavyo mazingira yanavyoweza kulindwa.
TIBA ASILI NI NINI?
TIBA ASILI ni Jumla ya maarifa na utendaji ambao unatumika katika kuchunguza, kukinga na kuponya ugonjwa wa kimwili, kiakili au kimahusiano ambao unategemea uzoefu wa kurithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo.

TIBA MBADALA NI NINI?
TIBA MBADALA ni Jumla ya maarifa na utendaji unaotumika katika uchunguzi, ukingaji na uponyaji wa matatizo ya kimwili, kiakili na kijamii na kutegemea tu mifumo mbalimbali iliyoanzishwa na Tiba Mbadala ya Nyanja husika.
Huduma hizi zitolewazo na watu waaina mbalimbali kwa kutumia nyenzo, ujuzi na uzoefu wa kiasili. Tiba asilia hutofautiana toka jamii au kabila moja hadi jingine. Baadhi ya dawa au Tiba toka jamii zingine zina ubora wa kipekee kiasi cha kuleta mvuto sehemu zingine.
MAZINGIRA NI NINI?
Mazingira ni vitu vyote vinavyotuzunguka vyenye uhai na visivyo na uhai. Vitu vyenye uhai ni pamoja na mimea na wanyama na visivyo ni pamoja na uhai ni hewa, ardhi na maji.

Mazingira yanahusisha pia vitu vyote vinavyosaidia kuendelea kuwepo kwa maisha ya mwanadamu na viumbe wengine. Hivyo basi maisha ya viumbe hai wa kizazi kilichopo na kijacho kinategemea uwepo wa mausiano mazuri kati ya watu na mazingira.

KAZI ZA MTABIBU WA TIBA ZA ASILI
Mtabibu wa tiba asili aliyepata mafunzo anatarajiwa kufanya yafuatayo:-
·       Kutunza kumbukumbu za wagonjwa kwa utaratibu unaokubalika.
·       Kutambua na kuhamasisha wagonjwa wenye vidokezo vya hatari na      wanaohitaji rufaa za mapema ili waende kwenye kituo cha afya husika kwa huduma ya utaaramu zaidi.
·       Kutoa huduma salama kwa kujari afya ya mgonjwa huku wakiwa wasafi.
·       Kutoa huduma katika mazingira ya usafi.
·        Kutoa elimu na nasaha kuhusu usafi, lishe bora na utunzaji wa mazingira.
• Kutoa dawa kwa utaratibu unaokubalika
• Kutunza vifaa vya huduma na dawa kwa utaratibu unaokubalika
• Kushirikiana na kuwaelewa watumishi wa afya
• Kupata mwanga juu ya misingi ya utafiti wa madawa ya asili.
• Kushirikiana na mashirika, vikundi vyama mbalimbali hususani vya kitaaluma.
• Kupambanua Watabibu wa kweli na tapeli
• Kutoa ushauri juu ya kupunguza kasi ya kuenea kwa magonjwa hususani magonjwa sugu kama kansa, kisukari, magonjwa ya zinaa na Ukimwi
• Kuzingatia sera, miongozo ya Serikali, sheria na kanuni na taratibu
za kitaaluma.
NAPENDA KUSISITIZA YAFUATAYO
(i) watoa huduma wa tiba asili – wachane na upingaji wa ramri zinazogonganisha/Kuchonganisha jamii na kukosesha amani ndani ya jamii.
(ii) Watoe tiba iliyo na tija kwa jamii ili tuweze kuokoa maisha ya
binadamu kwani watabibu wa tiba asilia mlishapewa karama na mwenyezi
Mungu kuokoa maisha ya watu, hivyo tutowe huduma itakayoendeleza Tiba asilia
(iii) Watabibu wa tiba asilia tunaitaji kuongeza elimu na bidii za utafiti wa madawa kwa ajili ya kutibu magonjwa mbalimbali yaliyoshindikana kutibiwa katika jamii zetu.
(iv)Pia wananchi tunaomba nasi tuachane na dhana potofu kwani nasi pia ni chanzo kikubwa cha kuleta ugomvi  kwa sababu unavyokwenda kwa mganga kutibiwa kuna tabia ya kulazimisha waganga wawambie wachawi wenu badala ya kuomba upatiwa dawa stahiki ya kutibu tatizo ulilonalo unayotokana na mimea asilia.

USAFI NA MAZINGIRA
(I) Mtoa huduma wa tiba asili anahitajika kwanza mwenyewe awe msafi wa mwili mzima kabla ya kuanza kazi, nguo zake za kazi ziwe safi, na mazingira yake yawe safi na salama kwa kutolea huduma ya tiba asilia.
Wagonjwa walazwe mahala pasafi, vyombo vya kuifadhia madawa na mahala pa kutunzia madawa pawe pasafi, vifaa viwe safi na salama. Pia anapo fanyia kazi pawe safi, vyoo viwili vyote viwe safi mabafu yote mawili yawe safi, hadi mavazi ya mganga mwenyewe yawe safi.
MADHARA YA UCHAFU
Unapokuwa unatoa huduma ukiwa mchafu basi unaweza kumuongezea mgonjwa wako magonjwa mengine, kumsababishia magonjwa ya kipindupindu, pumu, vikoozi vya kila wakati, ukimwi, pepopunda, funza, upele, ukurutu, kichocho na Ukimwi hatimaye kusababisha vifo vya watu.
WATABIBU TAPELI
Wapo watu wasiokuwa na uelewa juu ya Utoaji huduma ya tiba Aislia wanaodandia na kuchafua jina la taaluma ya tiba asilia ya kitanzania, wapo watu wasiokuwa na taaluma ya tiba asili au wanautambuzi mdogo sana kwa taaluma hii. Wapo wasioijua hii taaluma kazi yao ni kununua dawa kutoka kwa wataaluma, baadaye kujifanya kuwa wenyewe ndiyo wataaluma zaidi.
• Watu hao ni wasemaji sana.
• Hujipa sifa wenyewe
• Hujigamba sana
• Hujikweza
• Husema wana weza kutibu na kuponyesha kila aina ya ugonjwa.
• Ni wadanganyifu mno.
Hizo ni baadhi tu ya dalili za kutambua matapeli na wao wanajipenda sana zaidi ya mganga mwenyewe na gharama zao ni kubwa zaidi.
MAADILI YA TIBA ASILI
Watoa huduma za tiba asilia wanahitaji kuzingatia maadili ya dawa, kazi zao.
(i) Unahitaji kuelewa sera na sheria za 23/2002 ya tiba asili na tiba
mbadala Tanzania.
(ii) Kutunza siri za wateja wako
(iv)Kutokuwa na uongo na udanganyifu.
(v) Kutoendesha shughuli zako kiutapeli
(vi) Kutolewa wakati wa kutoa huduma.
(vii) Kutokubaliana na mteja kulipiza visasi
(viii) Kutopiga ramri za kuchonganisha
(ix) Kutonyanyasa wateja wako na kuwapiga,
(x) Timiza hivyo vipengele utaheshimika sana ndani ya jamii unamoishi.
FAIDA YA DAWA ZA ASILI
1. Inatibu na kuondoa magonjwa sugu
2. Inastawisha afya ya binadam zaidi
4. Ina boresha mwili wa binadam zaidi na ina virutubisho vingi.
Ndugu wananchi tunaomba tuzingatie utamaduni wetu na mila na desturi nzuri tusibaki kuthamini sana mila za kigeni Wananchi tugeuze akili zetu tutumie zaidi dawa zetu za asili ili tuweze kupunguza vifo vingi hapa nchini. Pia tule vyakula vya asili, mfano vyakula vyote vya nafaka na mafuta ya asili, mtaona mabadiliko ya nchi yenu kuwa makubwa kwa afya za binadam hata vifo vitapungua hapa nchini.
Mnaona magonjwa yanazidi kila kunapokucha na tiba hazipo zimebakia za wasiwasi. Nimatumaini kuwa wananchi watabadili fikira zao ili waokowe maisha yao.
Ahsante

IMETAYARISHWA NA KAMATI TENDAJI YA TRAMEPRO
CHINI YA KATIBU MKUU
……………………………
BONIVENTURA F. MWALONGO

KATIBU MKUU

TIBA ASILI TANZANIA NA SHIRIKA LA DAWA ASILIA NA ULINZI WA MAZINGIRA (TRAMEPRO)

TRAMEPRO ni Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira (Traditional Medicine and Environmental Protection Organization) lililosajiliwa chini ya Sheria ya Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali yaani Non – Govermental Organization (NGO’s) “Act 24 of 2002” lenye namba ya usajili 00NGO/00007772 linalofanya kazi kwa Karibu na Serikali na Jamii katika kufuatilia Matumizi sahihi ya dawa asilia , uandaaji wa dawa asilia, upatikanaji wa dawa asilia na uvunaji endelevu utakao pelekea kukua kwa pato la mtu mmoja mmoja na uchumi wa nchi pamoja na kulinda Mazingira ili kupata dawa asili iliyo na Virutubisho vya kutosha . Uvunaji makini wa Miti dawa utatuletea upatikanaji wa mvua za kutosha zitakazo tuwezesha katika kilimo, hewa safi, chakula pia kulinda na kuendeleza BAONUAI.

Dira ni kuwa na Jamii yenye kuheshimu, kutumia na kulinda Dawa za Asilia zinazotoka katika mazingira Asili na yaliyolindwa, ili kutuwezesha kuwa na Afya bora, kupambana na adui maradhi nakutambua vyanzo vinavyoweza kuchafua matumizi yetu Salama na kulinda usalama wa watumiaji.

Kwapamoja tunawajibu mbalimbali katika kuangalia upatikanaji na upandaji wa miti dawa ili kupata dawa kwa wingi na kuendelea kulinda Afya zetu na kutunza mazingira yetu. TRAMEPRO tunafanya juhudi mbalimbali za kuhakikisha jamii inapata elimu ya matumizi ya dawa asili na faida zinazopatikana kwa kulinda mazingira yetu .Ili kufanikisha matumizi sahihi ya Dawa asilia na kulinda Mazingira ni muhimu Kutoa Elimu na kuwajengea uwezo waganga, watabibu, wavunaji, wakulima, wazalishaji, wauzaji na Watumiaji wa dawa asilia.

TRAMEPRO kupitia semina, midaharo, makongamano mbalimbali tuliyoandaa na kushirikishwa (kushiriki), vipindi katika redio na television pamoja na mitandao yetu ya kijamii tumejitahidi kuelimisha matumizi sahihi ya dawa asilia na utoaji wa huduma sahihi za tiba asilia kwa matabibu kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu na miongozo iliyowekwa ili kuhakikisha kuwa jamii inakuwa na uelewa mkubwa juu ya matumizi sahihi ya dawa asili na kulinda mazingira yetu.        
     
Kwa kutambua Sera, Sheria, Kanuni, taratibu na miongozo inayo simamia shughuri zetu za kila siku na kushirikiana na wadau wa afya na Mazingira  hasa katika kufanya utafiti wa Dutu za mimea,wanyama, madini, ndege na wadudu tutakuza sekta yetu ya Tiba Asilia na Tiba Mbadala.

Leo tumekutana hapa na wadau mbalimbali wa Afya, Tiba Asilia, Tiba Mbadala na mazingira ili kujadili maelekezo na utekelezaji wa Maagizo ya Serikali ya tarehe 15 Januari 2016 yaliyotolewa na Mhe. Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto kwa watabibu wa Tiba Asili na Tiba Mbadala, kubadilishana uzoefu, ujuzi na maarifa kati yetu na wadu wengine juu ya njia bora na sahihi za kuwahudumia wagonjwa, ili kupunguza madhara yatokanayo na uzembe, ucheleweshaji na matukio mengine yanayoweza kusababisha ulemavu na vifo.

Pia kutoa elimu nasaha juu ya afya ya msingi kwa wateja wao, na kuleta uhusiano mzuri na wakaribu kwa wote, ikiwa ni pamoja na watabibu wa Tiba Asilia na Tiba Mbadala na jamii yote tukiwa na matarajio ya kuongeza upeo zaidi.
Shirika la dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira TRAMEPRO linaungana katika Mkutano huu ikiwa ni moja kati ya mikutano iliyoshiriki na kuandaa ili kupata maoni ya wadau  na kuongeza upeo zaidi juu ya huduma za Afya zinazotolewa kwa Tiba Asilia na tiba Mbadala na namna ambavyo mazingira yanavyoweza kulindwa.

TIBA ASILI NI NINI?
TIBA ASILI ni Jumla ya maarifa na utendaji ambao unatumika katika kuchunguza, kukinga na kuponya ugonjwa wa kimwili, kiakili au kimahusiano ambao unategemea uzoefu wa kurithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo.

TIBA MBADALA NI NINI?
TIBA MBADALA ni Jumla ya maarifa na utendaji unaotumika katika uchunguzi, ukingaji na uponyaji wa matatizo ya kimwili, kiakili na kijamii na kutegemea tu mifumo mbalimbali iliyoanzishwa na Tiba Mbadala ya Nyanja husika.
Huduma hizi zitolewazo na watu waaina mbalimbali kwa kutumia nyenzo, ujuzi na uzoefu wa kiasili. Tiba asilia hutofautiana toka jamii au kabila moja hadi jingine. Baadhi ya dawa au Tiba toka jamii zingine zina ubora wa kipekee kiasi cha kuleta mvuto sehemu zingine.
MAZINGIRA NI NINI?
Mazingira ni vitu vyote vinavyotuzunguka vyenye uhai na visivyo na uhai. Vitu vyenye uhai ni pamoja na mimea na wanyama na visivyo ni pamoja na uhai ni hewa, ardhi na maji.

Mazingira yanahusisha pia vitu vyote vinavyosaidia kuendelea kuwepo kwa maisha ya mwanadamu na viumbe wengine. Hivyo basi maisha ya viumbe hai wa kizazi kilichopo na kijacho kinategemea uwepo wa mausiano mazuri kati ya watu na mazingira.

KAZI ZA MTABIBU WA TIBA ZA ASILI
Mtabibu wa tiba asili aliyepata mafunzo anatarajiwa kufanya yafuatayo:-
·       Kutunza kumbukumbu za wagonjwa kwa utaratibu unaokubalika.
·       Kutambua na kuhamasisha wagonjwa wenye vidokezo vya hatari na      wanaohitaji rufaa za mapema ili waende kwenye kituo cha afya husika kwa huduma ya utaaramu zaidi.
·       Kutoa huduma salama kwa kujari afya ya mgonjwa huku wakiwa wasafi.
·       Kutoa huduma katika mazingira ya usafi.
·        Kutoa elimu na nasaha kuhusu usafi, lishe bora na utunzaji wa mazingira.
• Kutoa dawa kwa utaratibu unaokubalika
• Kutunza vifaa vya huduma na dawa kwa utaratibu unaokubalika
• Kushirikiana na kuwaelewa watumishi wa afya
• Kupata mwanga juu ya misingi ya utafiti wa madawa ya asili.
• Kushirikiana na mashirika, vikundi vyama mbalimbali hususani vya kitaaluma.
• Kupambanua Watabibu wa kweli na tapeli
• Kutoa ushauri juu ya kupunguza kasi ya kuenea kwa magonjwa hususani magonjwa sugu kama kansa, kisukari, magonjwa ya zinaa na Ukimwi
• Kuzingatia sera, miongozo ya Serikali, sheria na kanuni na taratibu
za kitaaluma.

NAPENDA KUSISITIZA YAFUATAYO
(i) watoa huduma wa tiba asili – wachane na upingaji wa ramri zinazogonganisha/Kuchonganisha jamii na kukosesha amani ndani ya jamii.
(ii) Watoe tiba iliyo na tija kwa jamii ili tuweze kuokoa maisha ya
binadamu kwani watabibu wa tiba asilia mlishapewa karama na mwenyezi
Mungu kuokoa maisha ya watu, hivyo tutowe huduma itakayoendeleza Tiba asilia
(iii) Watabibu wa tiba asilia tunaitaji kuongeza elimu na bidii za utafiti wa madawa kwa ajili ya kutibu magonjwa mbalimbali yaliyoshindikana kutibiwa katika jamii zetu.
(iv)Pia wananchi tunaomba nasi tuachane na dhana potofu kwani nasi pia ni chanzo kikubwa cha kuleta ugomvi  kwa sababu unavyokwenda kwa mganga kutibiwa kuna tabia ya kulazimisha waganga wawambie wachawi wenu badala ya kuomba upatiwa dawa stahiki ya kutibu tatizo ulilonalo unayotokana na mimea asilia.

USAFI NA MAZINGIRA
(I) Mtoa huduma wa tiba asili anahitajika kwanza mwenyewe awe msafi wa mwili mzima kabla ya kuanza kazi, nguo zake za kazi ziwe safi, na mazingira yake yawe safi na salama kwa kutolea huduma ya tiba asilia.
Wagonjwa walazwe mahala pasafi, vyombo vya kuifadhia madawa na mahala pa kutunzia madawa pawe pasafi, vifaa viwe safi na salama. Pia anapo fanyia kazi pawe safi, vyoo viwili vyote viwe safi mabafu yote mawili yawe safi, hadi mavazi ya mganga mwenyewe yawe safi.

MADHARA YA UCHAFU
Unapokuwa unatoa huduma ukiwa mchafu basi unaweza kumuongezea mgonjwa wako magonjwa mengine, kumsababishia magonjwa ya kipindupindu, pumu, vikoozi vya kila wakati, ukimwi, pepopunda, funza, upele, ukurutu, kichocho na Ukimwi hatimaye kusababisha vifo vya watu.

WATABIBU TAPELI
Wapo watu wasiokuwa na uelewa juu ya Utoaji huduma ya tiba Aislia wanaodandia na kuchafua jina la taaluma ya tiba asilia ya kitanzania, wapo watu wasiokuwa na taaluma ya tiba asili au wanautambuzi mdogo sana kwa taaluma hii. Wapo wasioijua hii taaluma kazi yao ni kununua dawa kutoka kwa wataaluma, baadaye kujifanya kuwa wenyewe ndiyo wataaluma zaidi.
• Watu hao ni wasemaji sana.
• Hujipa sifa wenyewe
• Hujigamba sana
• Hujikweza
• Husema wana weza kutibu na kuponyesha kila aina ya ugonjwa.
• Ni wadanganyifu mno.
Hizo ni baadhi tu ya dalili za kutambua matapeli na wao wanajipenda sana zaidi ya mganga mwenyewe na gharama zao ni kubwa zaidi.

MAADILI YA TIBA ASILI
Watoa huduma za tiba asilia wanahitaji kuzingatia maadili ya dawa, kazi zao.
(i) Unahitaji kuelewa sera na sheria za 23/2002 ya tiba asili na tiba
mbadala Tanzania.
(ii) Kutunza siri za wateja wako
(iv)Kutokuwa na uongo na udanganyifu.
(v) Kutoendesha shughuli zako kiutapeli
(vi) Kutolewa wakati wa kutoa huduma.
(vii) Kutokubaliana na mteja kulipiza visasi
(viii) Kutopiga ramri za kuchonganisha
(ix) Kutonyanyasa wateja wako na kuwapiga,
(x) Timiza hivyo vipengele utaheshimika sana ndani ya jamii unamoishi.

FAIDA YA DAWA ZA ASILI
1. Inatibu na kuondoa magonjwa sugu
2. Inastawisha afya ya binadam zaidi
4. Ina boresha mwili wa binadam zaidi na ina virutubisho vingi.
Ndugu wananchi tunaomba tuzingatie utamaduni wetu na mila na desturi nzuri tusibaki kuthamini sana mila za kigeni Wananchi tugeuze akili zetu tutumie zaidi dawa zetu za asili ili tuweze kupunguza vifo vingi hapa nchini. Pia tule vyakula vya asili, mfano vyakula vyote vya nafaka na mafuta ya asili, mtaona mabadiliko ya nchi yenu kuwa makubwa kwa afya za binadam hata vifo vitapungua hapa nchini.
Mnaona magonjwa yanazidi kila kunapokucha na tiba hazipo zimebakia za wasiwasi. Nimatumaini kuwa wananchi watabadili fikira zao ili waokowe maisha yao.
Ahsante

IMETAYARISHWA NA KAMATI TENDAJI YA TRAMEPRO
CHINI YA KATIBU MKUU
……………………………
BONIVENTURA F. MWALONGO

KATIBU MKUU

MWENYEKITI WA TRAMEPRO BWANA SIMBA ABDULRAHMAN SIMBA AKITOA SALAM ZA PONGEZI KWA MHE. DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KWA KUCHAGULIWA KUWA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SEND EMAIL TO TRAMEPRO

Name

Email *

Message *