-

.

.

TRAMEPRO

TRAMEPRO

NAIPENDA NCHI YANGU TANZANIA

Sunday 8 November 2015

NAHUU MDIO WASIFU WA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI

Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania tangu 2015-11-05 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John P. Magufuli,  alizaliwa  Oktoba 29, 1959  Wilayani Chato Mkoa wa Kagera ambayo hivi sasa ipo Mkoa wa Geita. Dkt. Magufuli amemuoa Mwalimu Janet na wamejaliwa
kupata watoto.
Kazi
Harakati zake za kisiasa zilianza mwaka 1995 alipogombea kiti cha ubunge katika jimbo la Chato na kuteuliwa kuwa Naibu Waziri katika Wizara ya Ujenzi. Mwaka 2000 Dkt. Magufuli aligombea na kushinda kwa mara ya pili  na kuteuliwa kuwa Waziri wa Wizara ya Ujenzi.  Katika chaguzi za mwaka 2005 na 2010, aliendelea kuwania  kiti cha ubunge katika jimbo la Chato na kushinda uchaguzi huo na kuteuliwa kuwa  Waziri wa  Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi hadi mwaka 2008 alipohamishiwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi, ambayo aliiongoza hadi mwaka 2010. Mwaka 2010 alipochaguliwa tena kuwa mbunge wa Chato aliteuliwa kuwa Waziri wa Ujenzi.

Elimu
Dkt. Magufuli pia alijiunga na Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) kwa mujibu wa sheria akianzia Makutupora, Dodoma (Julai - Desemba 1983), kisha akaenda kambi ya Makuyuni, Arusha (Januari hadi Machi 1984) na akamalizia katika kambi ya Mpwapwa mkoani Dodoma (Machi – Juni 1984). Mwaka 1985 alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam akisomea Shahada ya Sayansi ya Elimu akibobea kwenye masomo ya Kemia na Hisabati na alihitimu mwaka 1988. Kati ya mwaka 1991 na 1994  alijiunga na masomo ya Shahada ya Uzamili ya Sayansi katika Chuo Kikuu cha Salford nchini Uingereza, kikishirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambako alipata Shahada ya Uzamivu ya Kemia kati ya mwaka 2000 na 2009.

0 comments:

Post a Comment

MWENYEKITI WA TRAMEPRO BWANA SIMBA ABDULRAHMAN SIMBA AKITOA SALAM ZA PONGEZI KWA MHE. DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KWA KUCHAGULIWA KUWA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SEND EMAIL TO TRAMEPRO

Name

Email *

Message *