-

.

.

TRAMEPRO

TRAMEPRO

NAIPENDA NCHI YANGU TANZANIA

Friday 5 June 2015

WAZIRI MAHENGE ATOA TAMKO LA SIKU YA MAZINGIRA DUNIANI, TAREHE 5 JUNI 2015

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira Mhe. Dkt. Injinia Binilith Satano Mahenge akitoa tamko kuhusu wiki ya mazingira .
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Dkt. Binillith S.Mahenge amesema Tarehe 5 Juni ya kila mwaka watanzania tunaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani. Kitaifa Maadhimisho haya yataadhimishwa katika viwanja vya Tangamano, Mkoani Tanga.
Kimataifa kaulimbiu inayongoza Maadhimisho haya ni : "Ndoto Bilioni Saba. Dunia moja. Tumia Rasilimali kwa Uangalifu". (Seven Billion Dreams. One Planet. Consume with Care).

Ujumbe wa maadhimisho haya, unahimiza matumizi endelevu ya rasilimali zilizopo, ili kukidhi mahitaji ya idadi ya watu inayoongezeka duniani. Hivyo, ni muhimu kuwa na mikakati ya matumizi endelevu ya rasilimalizilizopo kwa faida ya kizazi cha sasa na kijacho.
Sote inatubidi kuchukua hatua mahususi za kuhifadhi misitu, uoto wa asili, vyanzo vya maji, maziwa, mito na mabwawa na kupanda miti. Aidha, tunahitaji kudhibiti, uchafuzi wa mazingira utokanao na shughuli za viwandani na umwagaji wa kemikali zenye sumu, utupaji wa taka ovyo, uchimbaji holela wa madini, uvuvi haramu, kilimo kisicho endelevu na shughuli za kibinadamu zisizoendelevu.
Tangazo hili limetolewa na Ofisi ya Makamu wa Rais kwa udhamini wa Kampuni ya Simu ya Airtel -Tanzania, katika kuadhimisha Siku ya Mazingira Duniani, ambayo Kitaifa itafanyika mkoani Tanga kuanzia tarehe 1 hadi 5 Juni, 2015.

0 comments:

Post a Comment

MWENYEKITI WA TRAMEPRO BWANA SIMBA ABDULRAHMAN SIMBA AKITOA SALAM ZA PONGEZI KWA MHE. DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KWA KUCHAGULIWA KUWA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SEND EMAIL TO TRAMEPRO

Name

Email *

Message *