-

.

.

TRAMEPRO

TRAMEPRO

NAIPENDA NCHI YANGU TANZANIA

Thursday, 23 June 2016

WATU WENYE UALBINO WASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA KUJENGA UELEWA KUHUSU ALBINO


 Watanzania wakishiriki kwenye matembezi ya Siku ya Kimataifa ya Kujenga Uelewa kuhusu Albino kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Juni 13, 2016. Baraza la Usalama la Umoja wa Matifa liliitangaza tarehe 13 ya kila mwaka kuwa iwe Siku ya Kimataifa ya Kujenga Uelewa kuhusu watu wenye Ualbino kwa nia ya kuondoa unyanyapaa, ukatili dhidi yao na kujenga heshima ya utu wa mtu.(PICHA ZOTE NA K-VIS MEDIA/KHALFAN SAID)
  Watanzania wakishiriki kwenye matembezi ya Siku ya Kimataifa ya Kujenga Uelewa kuhusu Albino kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam, leo Juni 13, 2016. Baraza la Usalama la Umoja wa Matifa liliitangaza tarehe 13 ya kila mwaka kuwa iwe Siku ya Kimataifa ya Kujenga Uelewa kuhusu watu wenye Ualbino kwa nia ya kuondoa unyanyapaa, ukatili dhidi yao na kujenga heshima ya utu wa mtu
 Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Anayeshughulikia masuala ya watu wenye ulemavu), Dkt. Abdallah Posii, akiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja kuongoza siku hiyo.
 Mtoto wa darasa la kwanza wa shule ya Jeshi la Uokovu, jijini Dares Salaam, Happy Simon (9), akilia baada ya kuimba wimbo unaotoa elimu kwa jamii kuwapenda na kuwalinda watoto wenye ualbino
 Dkt. Possi akimnyanyua mtoto Happy baada ya kuimba wimbo wake ambao ulisisimua wengi na kuinua hisisa kali
 Mmoja wa watu wenye ualbino, akisakata rhumba kutoka bendi ya Akudo Impacte waliokuwa na jukumu la kuburudisha hadhira
 Mfumaji mahiri wa kutumia shanga, Sophia Mohammed, (kushoto0, akimpatia maelezoNaibu Waziri Dkt. Possi (mwenye kofia) kuhusu ufundi wake na jinsi anavyojipatia kipato kwa kazi hiyo
 Mtoto huyu ni miongoni mwa watoto wengi waliohudhuria hafla hiyo
 Mama huyu mwenye ualbino akiwa amembeba mtoto wake, wakati wakiwasili kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
 Mama huyu akiwa na mtoto wake mwenye ualbino ni miongoni mwa waliohudhuria sherehe hiyo
 Afisa Mkuu Mtendaji wa Under The Same Sun, (UTSS), taasisi ya Kimataifa inayojishughulisha na utetezi wa watu wenye ualbino, Bi. Vicky Ntetema, (kulia), akifurahia jambo na wadau wake
 Mama huyu mwenye ualbino akiwa amembeba mtoto wake kwenye sherehe hizo
  Mama huyu mwenye ualbino akiwa amembeba mtoto wake kwenye sherehe hizo

Mama huyu akisubiri watu watembelee kwenye bidhaa zake
 Mtoto mwenye ualbino akishiriki matembezi hayo na mama yake
 Balozi wa Canada nchuini Tanzania, Alexandre Levique, (kushoto), Mwenyekiti Mtendaji wa IPP, Dkt. Reginald Mengi, (wapili kulia), na Maria Stanford, wakimsikiliza Afisa Mtendaji Mkuu, wa Shirika la Kimataifa linalotetea watu wenye Ualbino, Under The Same Sun (UTSS), Bi. Vicky Ntetema, wakati wa maadhimisho hayo
 Naibu Waziri Dkt. Possi naviongozi wengine kwenye meza kuu wakipokea matembezi ya maadhimisho ya sikuya kimataifa wa kujenga uelewa kwa watu wenye ualbino
Bi Ntetema (kulia), akitembelea moja ya mabanda ya biadhaa zinazotengenezwa na kuonyeshwa na watu wenye ualbino pamoja na wadau wengine

Friday, 10 June 2016

Rais Maguifuli atarajiwa kuwa mgeni rasmi siku ya Kimataifa ya Albino.

Rais Maguifuli atarajiwa kuwa mgeni rasmi siku ya Kimataifa ya Albino.

Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kuongeza uelewa kuhusu ualbino yatakayofanyika katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. Akiongea na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa chama cha Watu Wenye Ualbino Nchini (Tanzania Albinism Society) Nemes Temba ameeleza kuwa kupitia maadhimisho hayo jamii itapata fursa ya kupewa elimu muhimu kuhusu ualbino ili kuondoka na dhana potofu hususani ushirikina. “Maadhimisho haya ambayo yataanza Juni 11 hadi Juni 13, 2016 yatasindikizwa na mambo mbalimbali ikiwemo huduma za afya hususani uchunguzi na matibabu ya saratani ya ngozi pamoja na nasaha za viongozi na mabalozi, utambulisho wa Miss Albino Tanzania na uzinduzi wa kamusi ya ulemavu,” alisema Temba. Temba aliendelea kuainisha kwamba siku hiyo itawapa fursa watoto wenye ualbino waishio kwenye vituo mbalimbali nchini kutembelea mji wa Bagamoyo kujionea mambo mbalimbali chini ya ufadhili wa shirika la UNICEF. Aidha Mwenyekiti huyo amemshukuru Mhe. Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kuwapa vipaumbele watu wenye ulemavu akiwemo Dkt. Abdallah Possi ambaye ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Bunge, Sera, Ajira, Kazi na Watu Wenye Ulemavu hii inadhihirisha kuwa ulemavu si hoja bali utendaji kazi ndio kitu umuhimu. Mwenyekiti wa Jumuiya ya watu wenye Alibinism Tanzania (TAS) Nemes Temba akizungumza na waandishi wa Habari (hawapopichani) leo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujulisha umma siku ya maadhimisho ya Albino duniani.Kutoka kulia ni Mwenyekiti wa TAS Dar es Salaam, Gabriel Aluga, Katibu Mkuu wa TAS, Musa Katimba na Mratibu kutoka asasi ya kiraia ya BADEF. Mwenyekiti wa Mfuko wa Good Hope Star na mjumbe wa kamati ya maandalizi ya maadhimisho ya siku ya Albino duniani Al Shamaymaa Kwegyir akifafanua jambo wakati wa mkutano wa waandishi wa Habari (hawapopichani) leo jijini Dar es Salaam kwa lengo la kujulisha umma siku ya maadhimisho ya Albino duniani.Kutoka kuliani Mwenyektiwa TAS Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa TAS, Musa Katimba (kushoto) na Mwenyekiti wa TAS Taifa Nemes Temba.

Wednesday, 18 May 2016

NEW PARTNERSHIP TO ADDRESS INVESTMENT IN LAND TANZANIA.

Stakeholders in Tanzania’s land sector launch project to develop guidance for more socially responsible investment practices A new project aimed at ensuring investments in land and commodity procurement through supply chains are beneficial to local communities is launching in Tanzania today.


 The Responsible Investments in Property and Land (RIPL) project will develop country-specific, practical guidance tailored for use by investors, governments, and civil society organizations to equip each actor to engage in more gender sensitive and socially responsible investments.

These guidebooks will outline internationally recognized standards and principles, such as the African Union Guiding Principles, and take into consideration the
national governance framework and local context of Tanzania with the goal of improving investment
practices so all stakeholders can share more equitably in the benefits of land-based investments.
“The current, increased interest in large scale land investments in Tanzania holds great promise,” said
Joseph Olila director of the Tanzania Natural Resource Forum (TNRF). “But this wave of investment also
comes with risk. We know that 75 percent of Tanzanians live in rural areas and rely on land for their
livelihoods. Land is their most important asset and their claim to the land must be respected. This new
partnership, called the RIPL project, aims to provide all stakeholders with the tools they need to produce
successful and equitable outcomes for all parties – including women and men smallholder farmers.”
The civil society organization TNRF is leading the implementation of the project in Tanzania over the
next year. The project is being co-implemented with Landesa, a U.S.-based non-profit, with funding from
the UK’s Department for International Development (DFID). Wednesday’s project launch will bring
together representatives from both organizations, Tanzania’s Ministry of Lands and other land sector
stakeholders, including academics, civil society, and donors to discuss the project.
The RIPL project is conducting parallel work in Ghana being led by Ghanaian nongovernmental
organization Community Land Development Foundation (COLANDEF). 





Based on the country-specific guidance developed in both Ghana and Tanzania, the project plans to develop a model guidance . lick here to view the full pictures and press release http://tnrf.org/en/content/ripl-tanzania-press-release-18th-may-2016

Wednesday, 27 April 2016

Madhara ya kuchanganya dawa za hospitali na za asili

Image result for panadol

Wakati mwingine mwingiliano kinzani wa kiutendaji wa dawa za asili na zile za hospitalini, unaweza kusababisha dawa kugeuka kuwa sumu na kusababisha mzio hatari wa kuzimia na kushindwa kupumua.
Watu wanaougua magonjwa sugu wamekuwa wakijikuta kwenye mkanganyo kiasi cha kuwafanya watumie dawa za hospitalini pamoja na zile za asili bila kujua athari mbaya zaidi zitakazowapata. Matumizi ya dawa za asili au tiba mbadala kwa sasa yameenea sana. Za asili zinajizolea umaarufu sehemu mbalimbali duniani kutokana na kupigiwa debe muda mwingi




Dawa za asili.
Sheria za kimataifa zinapiga marufuku dawa za hospitalini kutangazwa kwa sababu mwenye mamlaka ya kuamua matumizi ni daktari na wala si mgonjwa Dawa za hospitalini hadi ziidhinishwe kwa matumizi ni lazima zipitie hatua mbalimbali kuthibitisha viwango vya kutibu, faida na hasara. Dawa za asili zimekuwa zikitumika ama kutokana na mazoea au mgunduzi kuzitangaza wakati athari zake zinazotokana na kiwango cha sumu kilichopo kutokujulikana.Pamoja na hali hiyo, jambo la hatari zaidi ni watu wengi kuchanganya dawa hizi za asili na zile zinazotengenezwa maalumu kutolewa hospitalini.Wagonjwa wengi hasa wenye magonjwa sugu yanayoelekea kushindikana hospitalini wanatumia tiba za asili kubahatisha uwezekano wa kupona. Wengine kwa kutokujiamini hujikuta wanaenda hospitali kupata dawa na wakati huo huo huenda kwa waganga wa jadi kupata huduma.Wengine wanapokwenda kuonana na madaktari, huwa hawako tayari kuweka wazi kwamba wanatumia dawa nyingine za asili.Kuna baadhi ya waganga wa jadi, kwa tamaa zao huwa wanawaambia wateja wao kuwa dawa zao haziwezi kuingiliana na zile za hospitali kwa kuwa ni kama chakula tu.
Ukweli ni kwamba nyingi zina sumu.Taarifa nyingi za kitabibu za hivi karibuni zinaonyesha kuwa wapo watu wengi wanaochanganya dawa hizi na kujikuta wanatengeneza tatizo jingine ambalo pengine ni kubwa zaidi ya lile linalowasibu.Katika utafiti huo, inaonekana kwamba madhara ya mwingiliano ama ukinzani wa dawa za asili na zile za kisasa, linaongezeka.Hata hivyo, taarifa hizi zinaweza kuwa hazitoi picha kamili kwa vile takribani asilimia 70 ya wagonjwa walioathirika, hawaelezi ukweli wa kuchanganya dawa.Kwa sababu hiyo hakuna utaratibu maalumu wa kuweka takwimu ili kufuatilia ukubwa wa tatizo hilo.
Dk Shufeng ZHOU aliandika makala kwenye jarida la ‘Herbal Medicine  Drug Interactions’ nchini Singapore, toleo la 6, akielezea juu ya utafiti wa matumizi mchanganyiko wa dawa za asili na zile za hospitalini.Dk Zhou anasema matumizi ya namna hiyo yanaweza kusababisha mwingiliano au ukinzani wa dawa na kusababisha madhara makubwa kwa mtumiaji.Matumizi ya namna hii yanaweza kuzuia dawa moja isifanye kazi, au moja iwe na nguvu zaidi kuliko kawaida na kudhuru mwili.Dawa zote zinaweza kujishikiza katika vipokeleo vya dawa vya aina moja na kushindana au kuzuia uzalishaji wa vimeng’enyo vya mwili visisafirishe dawa mwilini kama inavyotakiwa.Hali ya namna hii inaweza kusababisha usugu wa viini vya magonjwa hatari dhidi ya dawa mfano Viini vya Kifua Kikuu (TB), Virusi Vya Ukimwi (VVU), au kudhurika kwa ini na figo na kusababisha viungo hivi vya mwili, kushindwa kufanya kazi zake vizuri. Wakati mwingine mwingiliano kinzani wa kiutendaji wa dawa za asili na zile za hospitalini, unaweza kusababisha dawa kugeuka kuwa sumu na kusababisha mzio hatari wa kuzimia na kushindwa kupumua.Hatari ya mwingiliano kinzani wa utendaji wa dawa, huwa mkubwa zaidi pale dawa zaidi ya moja zinapotumiwa kwa pamoja.Mtafiti mmoja wa maswala ya dawa anasema kuwa, mtu anapotumia dawa mbili kwa wakati mmoja, hatari ya mwingiliano kinzani ni asilimia 6. Anapotumia aina tano za dawa mwingiliano ni asilimia 50 na hatari huongezeka zaidi hadi kufikia asilimia 100 pale mtu anapochanganya dawa nane au zaidi.
Hii ni kwa mujibu wa Kuhn Merrily, katika kitabu chake cha “Pharmacotherapeutics: A Nursing Process Approach. Philadelphia, Pa: FA Davis, 1998”.Dawa zinapoingiliana kiutendaji, hutengeneza mazingira yasiyofaa katika tumbo la chakula na utumbo, kiasi kwamba sehemu hizi za mwili hushindwa kufanya kazi ipasavyo. Matokeo yake ni kuharisha, kupata kichefuchefu au kupata vidonda vya tumbo au mwili kushindwa hufyonza kiasi cha kutosha cha dawa kwa ajili ya kupambana na ugonjwa. Mfano mzuri ni pale mtu anapotumia aloe vera na dawa za hospitalini kwa wakati mmoja anaweza kuharisha.
 Pia mwingiliano kinzani unaweza kusababisha dawa kujishikiza katika vipokeleo visivyo vya kawaida na kushindwa kusambaa kama inavyotarajiwa. Tatizo jingine hutokea wakati dawa zilizoingiliana kiutendaji zinapofika ndani ya ini. Hapo dawa huathiri vimeng’enywa vya ini vinavyoshughulikia dawa, vijulikanavyo kama CYP 450 enzymes na P-glycoprotein. Hali hii huweza kupunguza au kuongeza makali ya dawa kwa namna isiyokuwa ya kawaida.Hatari haiishii hapo, dawa zinapoingiliana kiutendaji pia huathiri utendaji wa figo na kushindwa kuondosha kiasi kikubwa cha sumu hatari mwilini. Hali hii inaweza kudhuru figo na kusababisha kiungo hicho muhimu kufa au kuwa dhaifu kiutendaji. Mwingiliano wa Dawa tunazotumia huathiri miili yetu kwa wema au kwa ubaya. Dawa zinapoingiliana kiutendaji zinaweza kupingana au kuongezeana nguvu na kuleta ufanisi au kuongeza makali ya dawa na kuwa sumu.  Baadhi ya dawa za asili zitokanazo na mimea huongeza makali ya dawa za hospitalini na nyingine hupunguza makali yake na kuvuruga kazi iliyokusudiwa ya kupambana na vimelea vya magonjwa Dawa za hospitalini pia huweza kuingiliana na zile za kufukiza, kupaka, kuchoma sindano au kuchanja. Madhara vile vile hutegemea kiasi cha dawa, maandalizi yake, umri wa mgonjwa, jinsia, maumbile ya vinasaba na aina ya magonjwa aliyonayo. Mfano kama una matatizo ya figo na ini, ni rahisi sana kudhurika kwa mwingiliano wa utendaji wa dawa. Mifano ya dawa zinazoingiliana Vitunguu saumu huingiliana na dawa za kupunguza makali ya VVU kama vile Ritonavir na Saquinavir Vitunguu saumu hupunguza nguvu ya dawa hizi kiasi kwamba mgonjwa anaweza kuwa na virusi vyenye usugu wa dawa hizo Vitunguu swaumu, tangawizi, mbegu na majani ya mpapai pamoja na bizari pia huongeza hatari ya mwili kushindwa kugandisha damu vinapotumiwa pamoja na dawa za hospitali.
Hii ni kutokana na kufanya damu kuwa nyepesi. Mshubiri (Aloe vera) unapotumiwa pamoja na dawa za moyo aina ya digoxin, huongeza hatari kwenye moyo kutokana na dawa hiyo asili kuwa na kawaida ya kuondoa madini ya potassium mwilini. Mshubiri una uwezo wa  kusababisha mtu kupata choo laini au kuharisha na kupoteza madini ya potassium. Ili moyo ufanye kazi vizuri unahitaji kiasi cha kutosha cha potassium.
Dawa za asili zitokanazo na Chamomile na Mpasheni zinaweza kuingiliana na dawa za usingizi za hospitalini na kuongeza hatari kwani nazo hufanya kazi ya namna hiyo. Dawa nyingi za asili zinaweza kuingiliana kiutendaji na dawa za kisukari, uzazi wa mpango na viuavijasumu. Hivyo ni muhimu kuchukua tahadhari kabla ya hatari. Jinsi ya kupunguza hatari Unapotumia dawa za asili ni vema kujua aina ya mimea iliyotumiwa kutengeneza dawa hizo. Unapotumia dawa za asili, anza na kiasi kidogo na kuongeza kwa kadiri unavyoona kuwa inafaa. Pia dawa za asili na za hospitalini zinapotumiwa sambamba ni bora kuachanisha muda wa kumeza au kutumia angalau kwa saa 3 hadi 4. Jambo jingine ambalo ni la msingi sana ni kumwambia daktari kama unatumia dawa za asili kabla hujapewa dawa za hospitalini.
 Ni busara kusimamisha dawa za asili siku 7 hadi 14 kabla ya kufanyiwa upasuaji, kujifungua au kung’oa jino. Hi ini kwa sababu baadhi ya dawa za asili hupunguza uwezo wa damu kuganda, hali ambayo ni hatari wakati wa upasuaji kwani damu inaweza kuvuja bila kikomo na kusababisha kifo. Lakini pia dawa zingine huingiliana na dawa za nusu kaputi na ganzi, jambo ambalo ni hatari kwa afya na maisha wakati wa upasuaji. Majani ni mmoja wa wataalamu katika Kituo cha utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Mbeya (NIMR-MMRC 0784 688 409
Stori na Clifford Majani, Mwananchi




Saturday, 26 March 2016

Usajili wa asasi,vyama, misikiti na vikundi wasitishwa


WAZIRI wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe ameuagiza Wakala wa Usajili, Ufilisi na Udhamini (RITA) kusitisha mara moja usajili mpya wa wadhamini wa asasi, vyama, misikiti na vikundi mbalimbali vya kijamii kwa lengo la kufanya uhakiki wa uhalali wa kuwepo wa taasisi hizo kisheria.
Ameagiza kuwa uhakiki huo ukamilike ndani ya miezi mitatu (siku 90) kuanzia sasa na orodha kamili ya wadhamini ikiwa ni pamoja na picha zao, anuani ya posta na makazi, na taarifa nyingine muhimu za utambuzi wa taasisi hizo mahali zilipo. Taarifa hizo ziwasilishwe Rita na nakala wizarani kwa uhakiki na kumbukumbu.
Dk Mwakyembe alitoa agizo hilo, alipokutana na watendaji na uongozi wa Bodi ya Rita, Dar es Salaam jana kwa lengo la kuboresha utendaji wa Wakala na kuendana na kasi ya Serikali ya Awamu ya Tano. Rita ina zaidi ya wadhamini 5,000 walio kwenye vitabu vyao vya usajili.
Aidha, Waziri huyo ameitisha kikao wiki ijayo cha mamlaka zote zinazohusika na usajili wa vikundi vya kijamii, mashirika, kampuni na asasi mbalimbali kwa lengo la kuimarisha taratibu za usajili na uendeshaji na kuboresha mawasiliano baina ya vyombo vya usajili vya dola ili kulinda maslahi mapana ya Taifa.

Saturday, 6 February 2016

RISALA YA MWENYEKITI WA WAGANGA WA MARUHANIA.


·        Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa
·        Afisa Maendeleo wa Mtaa
·        Mwenyekiti wa Kamati ya Afya na Mazingira
·        Wajumbe wa Serikali ya Mtaa
·        Mwenyekiti wa Maruhania
·        Katibu wa Maruhania
·        Waganga Mafundi, Walimu wa Maruhania (Watabibu wa Tiba Asilia)
·        Mabibi na Mabwana.
Habari za Muda huu
Leo ni siku ya pekee kwa wanamaruhania na watu wote wanaopenda maendeleo yetu na hasa katika tiba asilia na afya ya watanzania. Ni siku ambayo tunaandika historia katika Tiba Asilia na Maruhania. Kihistoria hakuna anayefahamu kwa hakika lini ushirikiano kati ya mwanadamu na Maruhani katika kutoa huduma ya Tiba Asilia na ilianza lini kutumika hapa kwetu Tanzania ila kila mmoja wetu atakubariana kuwa ilianza tuu pale binadamu wa kwanza alipoanza kuishi katika nchi yetu kwa miaka yote ya kuwepo kwa binadamu hapa Tanzania, Tiba ya kiruhani nayo imekuwa muhimili wa matibabu ya Tiba Asili.
Pamoja na kuwepo kwa maendeleo makubwa katika teknolojia na usambazaji wa huduma ya Tiba ya kisasa nchini kote lakini tiba ya maruhani asilia bado inaendelea kutumiwa na wananchi wengi, wa mijini na vijijini. Pamoja na Tiba ya kiruhani kutumiwa na wananchi wengi, huduma hii imekuwa ikitolewa katika mgumo usio rasmi, hali hii imekuwa ikichangia na kuifanya Tiba ya maruhani, isikubaliwe na watu wengi wasomi na Imani za mapokeo yasiyo ya asili ya mwafrika na mtanzania.
Kwakuwa serikali inatambua umuhimu wa Tiba Asilia hivyo kuanzia mwaka 1961 imekuwa ikichukuwa hatua mbalimbali kwa nia ya kuboresha huduma hiyo kwa kuweka sera, sheria, kanuni, miongozo na mikakati mbalimbali ya uendelezaji na uimalishaji.
Hatua hizo ni pamoja na kuanzisha taasisi za utafiti katika Tiba Asili, kuimalisha huduma za Tiba Asili kwa kuanzishwa kwa kitengo cha Tiba Asili, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Kujuishwa kwa Tiba Asili katika Sera ya Taifa ya Afya yam waka 1990, kutungwa kwa Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala Namba 23 ya Mwaka 2002 na Kuanzishwa kwa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kuanzia Mwaka 2005.
Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kwa Kushirikiana na Kitengo cha Tiba Asili, Imejikita katika Kutunga kanuni na Kutengeneza miongozo Mbalimbali ikiwa ni pamoja na utaratibu wa kuwasajili waganga na Wakunga wa Tiba Asili nchini ili kuimarisha utekelezaji wa Sheria namba 23 ya mwaka 2002, Sera, kanuni na Miongozo mbalimbali imekwisha sambazwa katika ofisi za waganga wakuu wa mikoa, wilaya,halmashauri za miji na Majiji na mpango wa maendeleo wa Afya ya Msingi wa mwaka  2007 – 2017.Vile vile Wizara imekuwa ikitoa elimu kuhusu Tiba Asili kupitia vyombo vya habari na maonesho ya kitaifa ya Tiba Asili na itaendelea kufanya hivyo.
Ndugu zangu wana Maruhani uhimalishaji wa Tiba Asili unajumuisha:-
·        Usajili wa Waganga, Wakunga na Wauza dawa wa Tiba Asili
·        Uanzishwaji na Usajili wa Vituo rasmi na Vilivyo bora vya kutolea huduma za Tiba Asili na Vinavyokidhi viwango vya Afya.
·        Utafiti na Utengenezaji wa Dawa unaokidhi viwango vya ubora, usalama na uwezo wa Kutibu.
·        Uanzishwaji wa kilimo cha miti dawa ili kuboresha dawa na mazingira.
·        Uwepo wa taratibu za usimamizi na udhibiti wa huduma ya Tiba Asili na Maruhania katika kutoa huduma ya Tiba Asili katika kila halmashauri ya Wilaya, Miji, Manispaa na Majiji.
Kwahiyo nawaomba kila Mganga wa Maruhania afuate maelezo yaliyotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya jamii, Jinsia Wazee na Watoto tarehe 15/ januari 2016, juu ya utolewaji wa huduma za Afya kwa Tiba Asili na Tiba Mbadala hapa nchini
hapa nchini kuna Sera, Sheria, Kanuni na Taratibu za maadili zinazotutaka tuzitii bira shuruti. Ni muhimu kwa kila mtoa huduma ya Afya kwa Tiba Asili ya Maruhani kutoa huduma kwa kuzingatia miongozo ya utoaji wa huduma hizo.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Watu wake wanathamini Tiba Asili na Tiba Mbadala, kwani Tiba Asilia ni Mama wa Tiba ya Kisasa. Sayansi ya Tiba ya Kisasa inatambua sayansi ya Tiba Asilia.
Hata hivyo huduma ya Tiba Asilia na Tiba Mbadala inakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na :-
·        kutotambuliwa na baadhi ya watoa huduma wa Tiba za Kisasa kwa sababu mitaala ya mafunzo ya wataalam wa Tiba za Kisasa(Madaktari, wafamasia na Manesi) imewanyima fursa ya kupata maarifa juu ya Tiba Asilia na matumizi yake katika tiba.
·        Katika Jamii pia kumekuwepo na Imani potofu kwa baadhi ya jamii wakihusisha Tiba Asilia na Imani za kishirikina.

·        Ukosekanaji wa fedha za Utafiti umesababisha kukosekana kwa utengenezaji wa dawa zinazokidhi viwango vya ubora, Usalama na Uwezo wa Kutibu na kuzisajiri dawa hizo kwenye mamlaka zinazohusika kwa mujibu wa Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo iliyopo.
·        Uhifadhi mbaya wa mashamba ya Miti dawa ili mitidawa hiyo iweze kufanyiwa utafiti na kuwa dawa bora na salama pamoja na utunzaji endelevu wa mazingira
·        Pia kunachangamoto ya  Uendelezaji wa Wataalam wa Tiba Asili kitaaluma ili wawe na uwezo wa kuboresha huduma zao baada ya kusajiliwa na Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Kukosekana kwa Muongozo wa ajira za utumishi katika sekta ya Tiba Asili.
Kama tulivyoahidi kuwa tutakuwa na mikutano ya uhamasishaji tunatowa shukurani kwa viongozi wa maruhani kuja kwenye mkutano huu na kujadiliana njia bora ya kufuata maelekezo ya Mhe. Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii,Jinsia Wazee na Watoto juu ya utowaji wa huduma ya Afya kwa Tiba Asili na Tiba Mbadala.
Walimu waambieni Maruhani kuwa Kuna agizo la Serikali linalotakiwa lifuatwe na Viti wao ili viti wao wasije wakapatwa na matatizo ya kisheria yaliyopitishwa katika nchi yetu ya Tanzania katika kutowa huduma ya Tiba Asili pia wafikishieni ujumbe huu watu wote walio na maruhani ambao wanatoa huduma ya Tiba Asili kwa kupitia Maruhani.
Ndugu viongozi wa koo za kiganga na mafundi wake, TRAMEPRO inataka viongozi wa koo za waganga wajitayarishe, tutaendelea na mkutano ya pamoja ili tutambike, ili waganga waliopo katika mila na desturi za kiganga wachukue fomu, kila mila itambike ili waganga wachukuwe fomu na kuanza kufuata utaratibu wa kisheria.
Baadhi ya makundi ya koo za kiganga na watoto wa dawa popote walipo tunataka viongozi wao, Walua, Wabisa, Waswezi, Watongwe, Ruhania, Waganga wa vitabu, Kidama, Kimbunga, Shimbalyoto, Kikola, Ndandi, Matepula, Mbei, lyamite, Shuma, Makamanda, Chambuya, Mchela, Kinyamkela, Lungu Likoko na koo nyingine zote.
Waganga tutowe huduma zetu kwa mfumo wa taasisi na siyo mtu mmoja mmoja kama ilivyo sasa kwa kuanzisha vituo rasmi kwa Mujibu wa Sheria, kanuni na Miongozo, ili iwe rahisi kupata mafunzo yanayostahili kwa huduma tunazozitoa kwa jamii.
Tayarisheni dawa katika sehemu maalum zenye mazingira ya usafi na salama ili kuepuka matumizi ya dawa zinazoweza kuleta madhara pamoja kutunza kumbukumbu kwa kuandika taarifa za ugonjwa na wagonjwa.
Tunaandaa mafunzo ya kuendeleza elimu na taaluma ya Tiba Asili ili mganga awe na uwezo wa kuboresha huduma azitoazo.
Kwa hivi sasa kutakuwa na uratibu wa kila Ngariba wanaotahiri wanaume ili wapate mafunzo maalum ya huduma waitoayo kwa jamii katika kulinda Afya ya Ngaliba mwenyewe na Muhitaji.
Waganga wa Tiba Asili, wauza duka la dawa asili, Wakunga wa Tiba asili, Ngariba wa wanaume, wenye viwanda vidogo vidogo vya utengenezaji wa dawa na wasaidizi wao tujisajiri kwa kipindi hiki cha miezi mitatu (3) na Vijijini tuzingatie miezi sita(6) tuliyopewa ili kuepuka hatua kali za kisheria zitakazo chukuliwa kwa kupuuza kusajiliwa katika kipindi kilichowekwa.
Shirika lenu la dawa asilia na ulinzi wa mazingira (TRAMEPRO) kwa kushirikiana na Watoa huduma wa Tiba Asili kwa ngazi zote , wasimamizi katika ngazi za maamuzi na wadau wote wa Tiba Asili tushirikiane kuitikia wito wa Serikali ili tuweze kupata na kutoa huduma zilizo bora na Salama.
Kwa changamoto zozote zitakazojitokeza katika kipindi cha kutekeleza agizo la Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, jinsia Wazee na watoto kwa Tiba Asili na Tiba Mbadala, tuwasiliane ili kupata ufumbuzi wa pamoja kabla ya muda haujamalizika yaani kabla ya Tarehe 15/April, 2016 kwa mjini na tarehe 15/Julai, 2016 kwa vijijini.
Lengo ni Kuona jamii ya watanzania inafikia malengo yake bila kuwepo kwa magonjwa, maisha bora kwaujumla kupitia dawa asilia na mazingira salama na yaliyotunzwa yanayo wazunguka.


ATHUMANI S. UNGANDO
MWENYEKITI, WAMARUHANIA

04/02/ 2016

Monday, 25 January 2016

MAELEZO YA WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA , WAZEE NA WATOTO KUHUSU TIBA ASILI NA TIBA MBADALA


Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu (katikati) akizungumza na waandishi wa habari, jijini Dar es Saslaam jana, juu ya serikali kupitia wizara hiyo kutoa msamaha wa miezi mitatu kwa waganga wanaotoa huduma za tiba asili na tiba mbadala kuendelea kujisajili ili kutambulika kisheria. Kulia ni Naibu waziri wa wizara hiyo, Dk.Hamis Kigwangwallah na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Dk. Mpoki Ulisubisya

WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO


MAELEZO YA WAZIRI KUHUSU TIBA ASILI NA TIBA MBADALA


Ndugu Wananchi, Katika nchi yoyote ile uhuru usio na mipaka ni jambo la hatari; lakini pia hakuna haki isiyo na wajibu. Vivyo hivyo, katika huduma za Tiba Asili na Tiba Mbadala hapa nchini kuna Sheria, Kanuni na Taratibu za Maadili zinazoweka masharti, uhuru na mipaka; pia haki na wajibu wa kila mdau. 

Huduma za tiba asili na tiba mbadala ni huduma zinazotambulika na Jamhuri yetu, watu wake na ina thamani kubwa. Aidha, ni huduma inayotambuliwa na sayansi ya tiba ya kisasa. Hata hivyo huduma hizo zimekumbwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuwepo kwa watoa huduma wasiozingatia Sheria, Kanuni na Miongozo mbalimbali. 

Kutokana na hali hiyo na kutokana na ziara ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamisi A. Kigwangalla (Mb) kwa Tabibu Juma Mwaka Juma tarehe 14/12/2015 na kufuatia uchambuzi uliofanywa na Wizara baada ya ziara hii, Wizara imebaini changamoto zifuatazo:-

1. Huduma za tiba asili na au tiba mbadala zinatolewa na watoa huduma wasiosajiliwa na Mamlaka husika kwa mujibu wa Sheria. 

2. Uwepo wa vituo vinavyotoa huduma za Tiba Asili na au Tiba Mbadala bila kusajiliwa kwa mujibu wa Sheria.

3. Kutolewa dawa kwa wagonjwa bila dawa hizo kusajiliwa na mamlaka husika. 

4. Uingizaji na matumizi ya vifaa vya uchunguzi ambavyo havijasajiliwa na mamlaka zinazohusika, na
5. Utoaji wa matangazo bila ya kufuatwa kwa matakwa ya sheria, Kanuni na Miongozo iliyopo. Aidha baadhi ya matangazo hayo yamekuwa na taarifa zinazoweza kuleta madhara na kupotosha Umma wa Watanzania.

Ndugu Wananchi,

Kutokana na hali hiyo, Wizara itahakikisha kuwa huduma za tiba asili na tiba mbadala zinatolewa kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Miongozo iliyopo. Lengo ni kuwezesha huduma za tiba asili na tiba mbadala zinakuwa huduma rafiki na salama kwa watumiaji. Tunao wajibu wa kuwalinda wananchi, vile vile tunaowajibu wa kuweka mazingira mazuri kwa watoa huduma za tiba asili na tiba mbadala ili kufanya shughuli zao vizuri.


Hivyo kwa upande wetu Wizara itahakikisha kuwa:- 

1. Baraza na sehemu inayosimamia huduma za Tiba Asili na Tiba Mbadala inakuwa na watumishi wa kutosha kwa mujibu wa Ikama. 

2. Kunakuwa na Mpango Mkakati wa muda mrefu kuwezesha kufanikisha uboreshaji wa huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini.

3. Watoa huduma wote, vituo vyote vya kutolea huduma, dawa na vifaa na vifaa tiba vinavyotumika vinasajiliwa. 

4. Utaandaliwa mwongozo wa mafunzo kwa watoa huduma wote nchini, kuhusu namna ya kuweka kumbukumbu za wagonjwa, kutoa rufaa kwa wagonjwa na kutengeneza dawa zilizo bora. 

5. Kunakuwa na mawasiliano na Wizara zinazohusika na habari na mawasiliano ili kuboresha utoaji matangazo yanayohusu Tiba Asili na Tiba Mbadala. 

6. Kunakuwa na mawasiliano na Ofisi ya Rais TAMISEMI na Taasisi za Utafiti ili kuboresha huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini. 

7. Tutafanya mabadiliko ya Sheria ili kuongeza kiwango cha adhabu kwa watakaokiuka, na pia tunakusudia kuondoa Kanuni inayoruhusu matangazo kwa idhini ya Baraza kwa sababu inaweka mianya ya matumizi mabaya ya fursa ndogo ya matangazo inayotolewa.
Ndugu Wananchi, Katika kufanikisha hayo, Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto inatoa maelekezo yafuatayo kwa watoa huduma na jamii:-

1. Hairuhusiwi kwa mtu yeyote kutoa huduma za tiba asili na au tiba mbadala bila kusajiliwa. 

Ninalielekeza Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala kuhakikisha kuwa watoaji huduma wote wanasajiliwa kwa mujibu wa Sheria: 
(a) Mijini, (Majiji, Manispaa na Miji) – usajili wao ukamilike katika kipindi cha miezi mitatu; kuanzia Januari 15, 2016 na 
(b) Vijijini, Halmashauri zote zilizobaki – usajili wao ukamilike katika kipindi cha miezi sita kuanzia Januari 15, 2016. Hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa yeyote atakaye puuza kujisajili katika kipindi hicho 

2. Hairuhusiwi kuuza na au kugawa dawa yoyote ile ya tiba asili au tiba mbadala mpaka iwe imesajiliwa na Baraza baada ya kuchunguzwa na Wakala wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali kuwa ni salama na kupewa kibali na Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA). 

3. Hairuhusiwi kuendesha kituo cha kutolea huduma za tiba asili na au tiba mbadala bila kukisajili. 

4. Wizara inapiga marufuku kwa mtu binafsi au taasisi yoyote ile kutumia kifaa au kifaa tiba chochote bila kukisajili TFDA na kupewa kibali; na 5. Matangazo yote yanayohusu Tiba Asili na Tiba Mbadala ambayo hayajapitishwa na Baraza yamezuiliwa kuanzia leo tarehe 15/1/2016. 

Wizara inavitaka vyombo vya Habari hasa Televisheni, Radio na Magazeti kuzingatia Sheria na Kanuni za Tiba Asili na Tiba Mbadala inayozuia matangazo ambayo hayajachunguzwa na Baraza. Ni wajibu wa vyombo vya habari kujiridhisha na Mamlaka husika yaani Baraza kabla ya kutoa tangazo lolote linalohusu Tiba Asili na Tiba Mbadala. 

Wizara itashirikiana na Mamlaka zinazohusika na habari na mawasiliano kutekeleza agizo hili. Vile vile, hairuhusiwi kutoa elimu kwa umma kupitia vyombo vya habari na mikutano ya hadhara kuhusu tiba asili na tiba mbadala.

Ndugu Wananchi, Katika kuwezesha ulinzi wa afya za wananchi, kila mmoja wote alinde afya yake kwa kuhakikisha kuwa huduma anayopata ya tiba asili na tiba mbadala ni kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Miongozo inayotolewa na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. 

Ni uhakika uliowazi kuwa kwa pamoja tukiboresha huduma za tiba asili siyo tu tutaboresha afya zetu bali pia tutaweza kuuza dawa na huduma hizo nje ya nchi na kupata fedha za kigeni kupitia na hivyo kuboresha uchumi wa mtu mmoja mmoja, jamii na nchi kwa ujumla.

Kwa pamoja tushirikiane kuboresha huduma za tiba asili na tiba mbadala nchini. 

INAWEZEKANA.

Ummy A. Mwalimu (Mb) WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO 15 Januari, 2016

MWENYEKITI WA TRAMEPRO BWANA SIMBA ABDULRAHMAN SIMBA AKITOA SALAM ZA PONGEZI KWA MHE. DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KWA KUCHAGULIWA KUWA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SEND EMAIL TO TRAMEPRO

Name

Email *

Message *