-

.

.

TRAMEPRO

TRAMEPRO

NAIPENDA NCHI YANGU TANZANIA

Sunday, 9 November 2014

BARAZA LA TIBA ASILI, MBADALA LAPIGA MARUFUKU MATANGAZO NA VIPINDI VYA TIBA HIYO

Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Profesa Rogassian Mahunnah.
Kutoka kushoto ni Kaimu Msajili wa tiba Asili Mboni Bakari, Mwenyekiti, Profesa Rogassian Mahunnah na Mfamasia Lucy Samweli.
BARAZA hilo limesema halitambui vipindi na matangazo yote ya tiba asili na tiba mbadala yanayoendelea kwa sasa kwenye vyombo vya habari nchini kwani ni batili yanapotosha na hayana vibali.
Baraza linawaomba wananchi kutokuamini huduma hizo ikiwamo za matumizi ya mashine za Quantim na zile za  kuondoa sumu mwilini, pamoja na  kuwataka waganga wanaotoa tiba hizo kujisajili ili kufanya kazi zao kihalali.
Hayo yamezungumzwa na Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala, Profesa Rogassian Mahunnah alipokuwa akizungmza na wanahabari katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam.
Kujua mengi zaidi tembela www.boresaclinic.blogspot.com

Friday, 31 October 2014

40 Images of Dubai; The city of Eccentricities


Dubai-Excentricidades-710x430
Dubai is one of the emirates that form the UAE (United Arab Emirates). Perhaps the most famous of the seven regions, and all because of two words; eccentricity and luxury. In less than thirty years, Dubai went from being the centenary fishing village to become one of the most distinctive and well-known cities of the planet.
In this collection of images we visit the famous city to understand how is Dubai, luxury and rich eccentrics. Clearly not everyone in the emirate are so rich than the persons you can see bellow, however, the images you see below are reason enough. I hope you will enjoy seeing these images.

Dubai was built in the desert, hence the palm trees…

Dubai-Palmera (3)
Dubai-Palmera

Course, are somewhat larger than normal. Even enters a luxury hotel on them…

Dubai-Palmera (2)
Dubai-Hotel

While that’s nothing in a place where everyone enters the world…

Dubai-Mundo
Dubai-Mundo (3)

the whole world? Sounds a bit overwhelming. Would be better if I go to a mall or a drink…

Dubai edificios (2)
Centro comercial-Dubai

Or the biggest garden of the world that only has 45 million flowers larger flowers… That’s it?

Dubai-Miracle

Maybe a coffee or a tea

starbucks-dubai

But first I will have to withdraw money from a vending machine for gold. Of course

Oro-Máquina

People of Dubai love gold, they have cars, shops  including dental prostheses made ​​of gold and diamonds. 24 carat gold and 156 small diamonds worth $ 153,000

Oro-Dubai (2)
Oro-Dubai
dub

In the end I decided to get a coffee, but I’ll have to rent a car; the place is extensive… and high

Aereo-Dubai
Dubai (2)
Dubai (3)

Dubai edificios

Now what I decide? Do I ask the car to the authorities?

Policia dubai

Or do I step through the parking lot of the American University in Dubai to see if it takes me a student?

Coches-Universidad-Dubai (2)
Coches-Universidad-Dubai (3)

I think it is best to go a with a sheikh

coches-Dubai (2)
coches-Dubai
Bugatti-oro
Bugatti-oro (2)

Well… maybe that’s a little dangerous. I didn’t know they love to go with their pets…

Dubai-Mascotas
Dubai-Mascotas (2)
Dubai-Mascotas (3)

I’d better grab one of these abandoned cars … yeah, that’s what I’ll do

Coche-Anadonado-Dubai
Coche-Anadonado-Dubai (2)

But it is very late… I’d better look for a hotel…

Hotel-Dubai (2)
Hotel-Dubai (3)
Hotel-Dubai (4)
Hotel-Dubai (5)
Hotel-Dubai (6)
Hotel-Dubai (7)
Hotel-Dubai (8)
Hotel-Dubai

So I can rest and lay off the day watching the biggest fireworks display that was ever made ​​in the world. This is how Dubai greeted 2014

Dubai 2014 firework display breaks world record
Dubai world record 2014
Dubai 2014 firework display breaks world record
Dubai-Fuegos Artificiales

Tuesday, 28 October 2014

TIBA ASILI ITAKAVYOTANGAZWA KIMATAIFA KATIKA MAONESHO YA TIBA ASILI YA MWAFRIKA November 16 hadi 25 Mwaka huu 2014

Tiba Asili itakavyotangazwa kimataifa
NA MWANDISHI WETU, Dar
KUANZIA Novemba 16 hadi 23 mwaka huu, kutakuwa na tukio la kihistoria katika Viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es Salaam. Kutafanyika Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Tiba Asili ya Mwafrika.
Maonyesho haya yanafanyika nchini kwa mara ya kwanza na yameandaliwa na Jukwaa la Tiba Asili Tanzania kushirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii na Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE).
Wadau mbalimbali wa Tiba Asili na Tiba Mbadala kutoka nje na ndani ya Bara la Afrika wanatarajiwa  kushiriki katika maonyesho hayo ambayo kauli mbiu yake ni ‘Ushirikiano wa Tiba Asili na Tiba za kisasa katika kuhimarisha huduma ya Afya Afrika’
Makundi makuu ya washiriki wa maonyesho hayo ni pamoja na Watabibu wa Tiba Asili, Watengenezaji wa Dawa Asili, Wakunga wa Tiba Asili, Kampuni za Dawa Asili na vipodozi vya dawa asili, Wasambazaji wa Tiba Asili na Tiba Mbadala, Watengenezaji wa vyakula asili, kliniki za Tiba Asili na Tiba Mbadala.
Kumekuwa na maoni mbalimbali kutoka kwa baadhi ya wadau wa Tiba Asili na Tiba Mbadala juu ya maonyesho hayo huku wengi wao wakisema kuwa yatatoa nafasi kwa wadau wa Tiba Asili na Tiba Mbadala kujitangaza kwa mapana zaidi.
Lakini pia kuna waliokwenda mbali zaidi na kusema kuwa kuna uwezekano mkubwa wa maonyesho hayo kuibua dawa nyingine za Tiba Asili kwa kujua ziko kwa nani, ni nani alifanya utafiti wa dawa hizo.
“Haya ni maonyesho ambayo yanatoa fursa pekee kwa watabibu na wadau wengine wa Tiba Asili na Tiba Mbadala kubadilishana mawazo kwa kile walicho nacho.
“Hii ina maana ya kwamba mshiriki kutoka Tanzania atajifunza jambo kutoka kwa mshiriki kutoka Uganga, Kenya na nchi nyingine zitakazoshiriki. Hii ndiyo faida mojawapo kwa wale watakaopata nafasi ya kushiriki katika maonyesho hayo,” alisema Simba A. Simba, ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Watabibu wa Dawa Asili Tanzania (ATME).
Hyasinta Ntuyeko ni muuzaji wa bidhaa za asili jijini Dar es Salaam ambaye anasema kuwa alipopata taarifa juu ya maonyesho hayo alivutiwa, akachukua fomu ya ushiriki akiwa anaamini kwamba ana kitu cha kujifunza kupitia maonyesho hayo.
 “Ni maonyesho mazuri kwasababu yatashirikisha watu kutoka nchi mbalimbali. Nafikiria kuwa hii ndiyo fursa pekee ambayo tunaweza kuitumia ikatujenga zaidi sisi wadau wa bidhaa za Tiba Asili na Tiba Mbadala,” alisema Hyasinta ambaye pia ni mtengenezaji na muuzaji wa taulo tiba za akina mama.
Innocent Oroki ni mmoja wa watengenezaji na wasambazaji wa dawa Asili kutoka Machame Moshi. Anasema kuwa anachofanya kwa sasa ni maandalizi ya dawa mbalimbali ambazo anataka watu wazione kwa wingi wakati wa maonyesho hayo.
“Kwa kuwa kupitia maonyesho haya tutapata fursa ya kuelimishana, nafikiri kwa upande wetu tumefikiria kuandaa dawa nyingi zaidi ili wenzetu kutoka nchi nyingine waweze kuziona na kutujua zaidi katika huduma hii ya Tiba Asili.
“Tiba Asili na Tiba Mbadala bado inahitaji kufahamika kwa watanzania walio wengi, Ninaamini maonyesho haya ni fursa muhimu kwetu kufanya hivyo kwa kuwapa elimu sahihi,” alisema Innocent
Lakini pia hakusita kuwakemea wale wanaotumia kofia ya tiba asili kufanya vitendo vinavyohatarisha maisha ya binadamu akidai kuwa hiyo ni moja ya changamoto kubwa ambazo bado wanahitaji kupambana nazo katika huduma ya Tiba Asili na Tiba Mbadala.  
“Changamoto nyingine kubwa tuliyonayo kwa sasa katika Tiba Asili na Tiba Mbadala ni baadhi ya watu wanaojiita watabibu wa Tiba Asili, kutumia mwavuli huo kufanya vitendo vya kuhatarisha maisha ya watu.
“Hili nalo tunahitaji kulikomesha kwa kuwaelimisha wananchi ili watambue na kufahamu mahala sahihi pa kupata huduma ya hizo kwa mujibu wa taratibu zilizowekwa na serikali,” alisema Innocent, ambaye hivi karibuni alikuwa jijini Dar es Salaam akifuatilia taratibu za kushiriki katika maonyesho hayo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya maonyesho hayo Boniventure Mwalongo anasema kuwa wanatarajia washiriki 280 kutoka nje na ndani ya nchi. Lakini pia anafafanua kuwa wamekuwa katika maongezi na taasisi na kampuni mbalimbali ambazo zimeonyesha kutaka kudhamini maonyesho hayo.
“Tuna maongezi na taasisi pamoja kampuni mbalimbali. Tayari baadhi zimekubali kutudhamini. Taarifa rasmi tutaitoa pale maongezi yatakapokuwa yamekamilika,” anasena Mwalongo.
Amewataka wadau wa Tiba Asili na Tiba Mbadala kujitokeza kwa wingi akielezea kuwa baada ya hapo watakuwa na mtandao mzuri wa wadau mbalimbali wa Tiba Asili na Tiba Mbadala katika Bara la Afrika.
“Kama maonyesho haya yamebeba jina la Afrika, basi hata sisi tutahakikisha tunajenga mtandao wa wadau wa Tiba Asili na Tiba Mbadala na hasa katika suala zima la kuhimarisha soko.
Kwa mujibu wa Mwalongo, gharama za kushiriki zimegawantika katika makundi tofauti ambapo Watambuzi wa magonjwa, watengenezaji wa dawa asili, wakunga wa tiba asili, Wenye virutubisho vya tiba asili na  wauzaji wa dawa asili gharama yao ni 100,000/-. Kampuni za dawa asili na vipodozi asili zitalipa 500,000/-.
Wasambazaji wa dawa za asili na dawa mbadala watatakiwa kulipa ada ya 1,000,000/-. Wauza vyakula asili  watalipia 150,000/- wakati kliniki ya tiba asili watalipia 1,500,000/- Kliniki ya tiba mbadala gharama yake ni 2,000,000/-. Kampuni za virutubisho kutoka nje ya Jumuiya ya Afrika Mashariki zitalipia  dola za Marekani 1,500.
Viwango vingine ni dola 500 za Marekani kwa Kampuni za Tiba Asili ndani ya Jumuiya ya Afrika Mshariki. Gharama za ushiriki kwa Benki, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Taasisi za Serikali ni 2,000,000/-. Wajasiliamali wa kazi za uchongaji watalipia 500,000, wakati vyama vya tiba asili vitalipia 1,000,000.
Aidha Mwalongo alitoa wito kwa makundi mengine ambayo yangependa kushiriki, kujitokeza mapema ili taratibu ziweze kufuatwa. “Huenda kuna makundi mengine ambayo labda tumeyasahau, lakini milango bado iko wazi kwa yeyote ambaye angependa kushiriki maonyesho haya,” alisisitiza Mwalongo.
Alisema kuwa wana imani baada ya maonyesho hayo kutakuwa na mtandao mkubwa wa kibiashara katika huduma ya tiba asili na tiba mbadala kwa nchi za Afrika na hata nje ya Afrika. Aidha alisema kuwa wako mbioni kuyasajili rasmi maonyesho hayo ili yawe yanafanyika kila Agosti 30 pale inapoadhimishwa siku ya Tiba Asili ya Mwafrika.

Saturday, 18 October 2014

JUKWAA LA TIBA ASILI TANZANIA KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII NA MAMLAKA YA MAENDELEO YA BIASHARA TANZANIA (TANTRADE) LINATOA TANGAZO KUWA:


                                   TANGAZO

JUKWAA LA TIBA ASILI TANZANIA KUSHIRIKIANA NA WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII NA MAMLAKA YA MAENDELEO YA BIASHARA TANZANIA (TANTRADE), LIMEANDAA MAONYESHO YA KIMATAIFA YA BIASHARA YA TIBA ASILI YA MWAFRIKA YATAKAYOFANYIKA VIWANJA VYA MNAZI MMOJA JIJINI DAR ES SALAAM KUANZIA NOVEMBA 16 -23, 2014. WATOA HUDUMA YA TIBA ASILI NA TIBA MBADALA PAMOJA NA WANANCHI WOTE MNAKARIBISHWA KUPATA HUDUMA NA MAARIFA YA TIBA ASILI.
LENGO LA MAONYESHO HAYO NI KUWALETA PAMOJA WATAALAMU NA WADAU MBALIMBALI WA TIBA ASILI BARANI AFRIKA KUJENGA MTANDAO WA PAMOJA KATIKA KUBORESHA HUDUMA YA TIBA ASILI.
MAONYESHO HAYO YAKO WAZI KWA WAFANYABIASHARA NA KAMPUNI NYINGINE ZITAKAZOTAKA KUSHIRIKI.
KWA MAWASILIANO PIGA SIMU NAMBA

Sunday, 28 September 2014

TIBA ASILI BADO IMEGUBIKWA NA CHANGAMOTO

   AGOSTI 31 mwaka huu kulikuwa na Maadhimisho ya Siku ya Tiba Asili ya Mwafrika yaliyofanyika Zanzibar katika viwanja vya Bustani ya Victoria mjini humo.
Moja ya mambo yaliyosisitizwa na Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein, kupitia hotuba yake iliyosomwa na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad, ni pamoja na kukemea baadhi ya watu kisiwani humo wanaojitangaza kupitia baadhi ya misikiti na mabaraza kuwa wana uwezo wa kutoa Tiba Asili, akisema kufanya hivyo ni kinyume na sheria.



Lakini pia hakusita kusema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inalipa kipaumbele suala la utafiti wa Tiba Asili na kuwa kuna uhusiano mzuri kati ya Wizara ya Afya na chama cha Watabibu Asili visiwani humo. Mwisho akaagiza mamlaka husika kushughulikia tatizo hilo.

Caroline mtafiti  wa tiba Asili kutoka chuo kikuu cha Berlin Ujerumani akipata maelezo kutoka kwa Mtabibu na Mtafiti wa Tiba Asili Bwana Boniventura Mwalongo ambaye pia ni Katibu wa ASSOCIATION OF TRADITIONA AND ALTERNATIVE MEDICINE IN EAST AFRIKA kutoka Tanzania  
Awali akisoma hotuba yake katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala Zanzibar, Mayassa Salum Ally Alisema kuwa Wizara ya Afya kupitia baraza hilo imefanya jitihada mbali mbali kuinua Tiba Asili na Tiba Mbadala na kufanikiwa kuongeza idadi ya wataalamu hao ambapo sasa kuna watabibu 193 waliosajiliwa na kuna jumla ya kliniki 18 na vilinge  125.

 Rais wa chama cha Tiba Asili na Tiba Mbadala Afrika Mashariki Lyidia Matoke Akitoa Maelezo kuhusu Tiba Asili Kwa Makamu wa Kwanza wa Rais  wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad

Sera ya Taifa ya Afya inaonyesha kuwa kabla ya Uhuru, huduma za afya zilikuwa zikitolewa zaidi katika maeneo ya shughuli za kiuchumi kama miji na mashanba makubwa. Baada ya Uhuru serikali iliweka msukumo zaidi katika kupanua huduma za afya ili kuwafikia wananchi walio wengi, hasa walioko maeneo ya vijijini.
Tiba Asili na Tiba Mbadala imekuwa ikishika kasi kila kukicha, japokuwa kuna changamoto za hapa na pale. Kuna haja ya kukubali kuwa changamoto nyingi zinazotokea katika eneo hili la Tiba Asili na Tiba Mbadala huenda zinatokana na ukosefu wa elimu ya kutosha kwa watanzania walio wengi ambao mara nyingi wamekuwa wakishindwa kutofautisha Tiba Asili na tiba nyingine zinazotolewa kwa kisingizio cha mtindo huo.
Kutokana na mkanganyiko huu, kumekuwa na tafsri za aina tofauti juu ya aina za waganga. Katika imani za kawaida, kuna aina tatu za waganga: Waganga wa Asili, Waganga wa Jadi na Waganga wa Kienyeji.
Kutokana na tafsiri inayotolewa na Chama Cha Utabibu Asili Tanzania (ATME),  Mganga wa asili ni yule anaye shughulika na tiba za maradhi kwa kutumia dawa za asili, kutibu maradhi  kwa binadamu, wanyama mimea kwa kufuata maadili ya utoaji huduma ya matibabu
Mganga wa Jadi: Anatumia Mila na Desturi katika tiba na utoaji dawa kwa wagonjwa iwe binadamu, wanyama, mimea. Hutegemea zaidi mila na desturi pamoja na tiba asili na dawa za asili kama kanuni na maadili ya utoaji huduma ya tiba.

Mganga wa kienyeji: Hana mafunzo maalumu ya tiba ya upande wowote wa tiba katika utoaji wake wa huduma kwa jamii. Ni mtu anayeweza kuchanganya taaluma mbalimbali hata za kisayansi ili mradi afanikishe alichokusudia. Mganga huyo pia anaweza kutumia vazi lolote liwe la Sheikh, Askofu, Daktari, Mganga wa Asili, ilimradi afikie lengo lake.

ATME wanasisitiza kuwa, mganga yoyote mwenye fani nzuri akiitumia katika kutenda maovu, huyo ndiye mganga wa kienyeji na wala si mtaalamu wa Tiba za Asili.
Kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), takribani 60% ya wananchi huanza kutumia tiba asilia wanapopatwa na maradhi kabla ya kwenda vituo vya kutolea huduma za afya.
Nchini Tanzania Tiba Asili imekuwa na changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni ile ya baadhi ya watu kuihusisha na vitendo vya kishirikina, hali ambayo ni kinyume na sheria na taratibu zake, lakini pia kupotosha jamii.
Kwa mujibu wa Sheria ya Tiba Asili na Tiba Mbadala ya mwaka 2002, watabibu wote wa Tiba Asilia na Mbadala wako chini ya Baraza la Tiba Asili na Tiba Mbadala ambalo mbali na majukumu mengine lina jukumu la kusajili watabibu wote wenye sifa zinazotakiwa baada ya kuwafanyia usaili. Lakini pia kuendeleza na kuboresha huduma hiyo.
Moja ya mikakati ya Baraza hilo kwasasa ni kuhakikisha kuhakikisha kuwa watabibu wote wa Tiba Asili wanapata usajili, ili kudhibiti vitendo vinavyotishia maisha ya binadamu ambavyo vimekuwa vikihusishwa na Tiba Asili.
Baraza linakiri kuwa ni kweli kuwa kuna idadi kubwa ya watu anbao wanajihusisha na huduma ya tiba asili kinyemela, kitu ambacho ni kinyume na sheria. 
Katika semina ya vyombo vya habari iliyoandaliwa na ATME jijini Dar es Salaam Mei 15 mwaka huu katika Ukumbi wa NMR Dar es Salaam,  Mlezi wa chama hicho, Kingunge Ngombale Mwiru alisema Watanzania wengi ni wazito  kukubaliana na Tiba Asili, hali ambayo alisema inachangiwa na dhana ya kutawaliwa na wakoloni.
Mwenyekiti wa ATME Simba Abdulhamani Simba anasema kuna umuhimu wa serikali kuhakikisha kuwa watabibu wote wa tiba asili wanasajiliwa ili kupunguza matukio ambayo yamekuwa yakifanywa na baadhi ya watu wanaojiita wataalamu  wa tiba, lakini kwa kuichanganya na vitendo vya kishirikina.
Boninventure Mwalongo ni Mkurugenzi wa Kliniki ya Tiba Asili ya Boresa ya jijini Dar es Salaam ambaye pia ni Mratibu wa ATME, anasema kuwa kwa sasa wako katika mkakati wa kuhakikisha wanawashirikisha wadau mbalimbali ili jamii itambue umuhimu

wa tiba asili, ikiwa ni pamoja na kutoa semina kwa wadau mbalimbali.

Mwalongo anasema kuwa jambo jingine ambalo linatakiwa kudhibitiwa ni matangazo holela ya waganga ambayo yamekuwa yakibadikwa na hata mengine kutumika katika vyombo vya habari bila kufuata utaratibu.
Aidha kumekuwa na uhusiano wa karibu kati ya wadau wa Tiba Asili na Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini (TFDA). Mwaka 2012 kulikuwa na mkutano wa wadau wa dawa za asili. Halikadhalika Novemba 5 mwaka jana TFDA walikutana tena na wadau wa Tiba Asili.
Moja ya malengo ya mkutano huo ilikuwa ni pamoja na kukumbushana matakwa ya sheria pamoja na changamoto za udhibiti. Katika Mkutano huoMkurugenzi Mkuu waTFDA, Hiiti Sillo alisema kuwa moja ya changamoto katika Tiba Asili na Tiba Mbadala ni kuwepo katika soko bila kufuata taratibu za utengenezaji, lakini pia akasema akaongelea juu ya baadhi ya watu kutoa matangazo katika vyombo vya habari pasipo vibali vya Mamlaka hiyo.
Mwalongo anasema kuwa mikutano kama hiyo inadhihirisha jinsi Tiba Asili inavyozidi kupata uigo na kuzidi kuthaminiwa na kwamba watanzania wanapata mwanga zaidi wa kutambua kilicho bora na kuepuka udanganyifu kwa baadhi ya watu wanaojiita watabibu asili kinyume na utaratibu.
“Kwa ushirikiano kama huu nafikiri tutafika mahala watanzania walio wengi watafahamu umuhimu wa Tiba Asili kama ilivyo katika nchi za India na China ambako kwa mujibu wa takwimu za nchi hizo asilimia 80 za raia katika nchi hizo wanategemea Tiba Asili.
Ends.

MWENYEKITI WA TRAMEPRO BWANA SIMBA ABDULRAHMAN SIMBA AKITOA SALAM ZA PONGEZI KWA MHE. DKT JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KWA KUCHAGULIWA KUWA RAISI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

SEND EMAIL TO TRAMEPRO

Name

Email *

Message *