TRADITIONAL MEDICINE AND ENVIRONMENTAL
PROTECTION
SHIRIKA LA DAWA ASILIA NA ULINZI WA MAZINGIRA
TAMKO LA KATIBU MKUU WA TRAMEPRO KUHUSU WATOTO
WALIOMALIZA ELIMU YA MSINGI LILILOTOLEWA TAREHE 10/09/2016
Ndugu Waandishi wa Habari,
Katika jamii yoyote ile duniani watoto wote bila kujali kabila,
mila, rangi, utaifa,dini, jinsia, ulemavu, hali ya kiuchumi, ukimbizi au hali
yoyote , moja ya haki na urithi pekee wenye thamani kwao ni Elimu. Elimu
humfanya mtoto aweze kujitambua na kumpa upeo utakaomuwezesha kukabiliana na changamoto
mbalimbali za kimaisha ili aweze kuishi vyema katika maisha yake ya hapa
duniani.
Nitumie fursa hii kuwapongeza watoto wote waliomaliza mtihani wa
Taifa wa kuhitimu Elimu ya Msingi mwaka huu wa 2016, PONGEZI SANA! Ni jambo muhimu
kama wazazi/ walezi na Taifa kwa ujumla kwani hii ni fursa adimu kwa ustawi na
maendeleo ya mtoto na ni miongoni mwa njia ya kutimizwa kwa haki ya msingi ya mtoto
ya kuendelezwa ambayo inamjengea mtoto msingi imara wa maisha yake ya baadae.
Ndugu Wanahabari, TRAMEPRO tunaipongeza Serikali ya Jamhuri ya
muungano wa Tanzania kwani Takwimu zinaonyesha kuwa, wanafunzi 795,761
(wavulana 372,883 sawa na asilimia 46.86 na wasichana 422,878 sawa na asilimia
53.14) wamesajiliwa kufanya mtihani wa darasa la saba mwaka huu.
Ni matarajio yetu kuona watoto wote wanapata nafasi ya elimu ya
Sekondari kwakuwa Msingi tayari umeshawekwa na Serikali yetu tukufu ya Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania chini ya Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli wa kutoa na
imekusudia kumpa kila mtoto Elimu ya Sekondari bure. Hivyo tusingefurahi
mmojawapo kati ya watoto hawa waliomaliza elimu ya msingi akaikosa nafasi hii
kwa sababu zinazoweza kuzuilika
Hivyo ningependa kutumia fursa hii pia kuwaasa watoto
waliomaliza darasa la saba kutojihusisha na tabia au vitendo vyovyote vinavyo
hatarisha afya, usalama na maendeleo yao, kama vile kujihusisha kwenye masuala
ya ngono, matumizi ya madawa ya kulevya na vileo katika kipindi hiki cha
kusubiri matokeo ya mitihani yao.
Watoto wetu wa Kike na Kiume wajitambue, na wajue kuwa wao
ni hazina ya pekee katika maendeleo ya nchi yetu. Kipindi hiki wakitumie vizuri
kwa kuwa waadilifu, waaminifu, wenye bidii na kuzingatia kanuni za nidhamu na
tabia njema huku wakijiandaa kwa ajili ya kuendelea na elimu ya Sekondari.
Ndugu waandishi
Pamoja na juhudi nzuri ya serikali ya kuhakikisha elimu
inapatikana bure kwa watoto wote kuanzia shule ya msingi hadi sekondari, lakini
bado kunawananchi wengi hawajapata elimu nzuri na yakutosha kwa kuhusha elimu
na mambo ya ushirikina. Hari hiyo hupelekea kukwamisha maendeleo ya elimu kwa
watoto na hasa maeneo ya vijijini
Kwa waganga wachache wasiokuwa waaminifu wasiofuata maadili
katika utabibu kuihusisha tiba asili na ushirikina. Hali ambayo huchochea
umasikini na kukwamisha maendeleo ya elimu
TRAMEPRO inapenda kuwaasa wazazi, walezi na watoto
kuwaasa watoto wote kutumia kipindi hiki kwa kukataa kurubuniwa,
kushawishiwa na kujiingiza katika mambo yenye kuhatarisha afya, usalama na
maendeleo yao.
TRAMEPRO inawataka Wazazi Walezi Watoto na jamii kwa ujumla:-
1.
Kuwashirikisha watoto
katika shughuri mbalimbali za usafi na ulinzi wa mazingira katika kipindi hiki
cha kusubiria matokeo yao na isiwe Kuwaozesha watoto wa wao waliohitimu darasa
la saba kwa sababu yoyote ile au kwa lengo la kujipatia mali kwa njia ya
mahari.
2.
Kuwashirikisha watoto
kupata maoni yao, kujiunga na vikundi mbalimbali vya stadi za maisha, kama
michezo kusikilizwa na kushiriki kwa
hiari yake katika maamuzi yahayohusu maisha yake kulingana na umri na upeo
wake.
3.
Kuwapa uhuru watoto wa
kujifunza asili yao, tamaduni zao kwa kuwaelimisha kutofuata matembo mabaya
yanayofanywa na baadhi ya wanajamii kwa mfano kujiepusha na jamii zenye Imani potofu
kama unyanyapaa kwa watu wenye ualbino.
4.
Kuwaasa watoto
kujiepusha na kuingia kwenye mahusiano ya kimapenzi wakiwa na umri mdogo pamoja
na kuwapa elimu juu ya magonjwa ya kuambukiza na mimba katika umri mdogo. Kwa mujibu wa Sheria ya makosa ya kujamiiana
ya mwaka 1998 ambayo imefanyiwa marekebisho na kuhuishwa kwenye Makosa ya Jinai
(Penal Code Cap 16) inaelekeza kuwa ni kosa la jinai kwa mtu yoyote
kumlaghai mtoto wa umri wa chini ya miaka 18 kwa kumpa mimba au kufanya
nae mapenzi.
5.
Pia tunapenda kuwaasa
watoto kujiepusha na matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii na kwa wazazi
kutotoa fursa kwa watoto kutumia vibaya mitandao ya kijamii
Lengo ni kuona jamii ya watanzania inafikia malengo yake kwa kutokomeza
umaskini, ujinga na maradhi kwa kuwatimizia watoto haki ya elimu ili waweze
kutimiza ndoto zao na kulijenga taifa letu la Tanzania
Imetolewa na:-
BONIVENTURA F. MWALONGO
KATIBU MKUU WA TRAMEPRO
DAR ES SALAAM
10/09/2016
0 comments:
Post a Comment