|
Ugonjwa wa Homa ya Manjano husababishwa na virusi ambavyo huenezwa
na mbu aina ya `Aedes` ambaye huweza kuvichukua virusi kutoka kwa wanyama aina
ya nyani au kutoka kwa mtu mwenye ugonjwa huu na kuambukiza mtu mwingine kwa
kumuuma.
Pamoja na kueneza virusi vinavyosababisha Homa
ya Manjano (Yellow Fever), mbu huyu pia
huweza kueneza virusi vinavyosababisha Homa ya Zika, Homa
ya Dengue na Chikungunya. Hivyo udhibiti wa Mbu huyu aina ya Aedes unachangia sana katika kudhibiti
magonjwa haya kwa pamoja.
Ndugu Wananchi,
Dalili za mtu mwenye ugonjwa wa Homa ya Manjano ni pamoja na kuwa
na homa, kuumwa na kichwa, maumivu ya misuli pamoja na mgongo, mwili
kutetemeka, kupoteza hamu ya kula, kusikia kichefuchefu, kutapika na mwili kuwa na rangi ya manjano.
Dalili nyingine ni kutokwa na damu sehemu za wazi kama mdomoni,
puani, machoni na masikioni. Pia wakati mwingine damu huonekana kwenye
matapishi, kinyesi na figo kushindwa kufanya kazi. Kipindi cha kuonekana kwa
dalili za ugonjwa huu ni kati ya siku 3 hadi 6 baada ya kuambukizwa.
Ndugu Wananchi,
Ugonjwa wa Homa ya Manjano
hauna tiba kamili na hivyo mtu akiupata anaweza kupoteza maisha kama hajapata
huduma za afya mapema. Hata hivyo, ugonjwa huu una chanjo ambayo mtu akipata
humkinga asipate maambukizi.
Chanjo hii imethibitishwa na Shirika la Afya Duniani (WHO) kuwa na uwezo wa
kukinga mtu dhidi ya maambukizi ya virusi kwa kipindi chote cha maisha yake.
Hii ina maana kuwa hivi sasa mtu akipata chanjo hiyo mara moja itatosha
kumkinga kwa maisha yake yote.
Ndugu
Wananchi,
Kama mnakumbuka tarehe 21 Machi 2016 nilitoa
tamko la tahadhari ya ugonjwa wa Homa ya Manjano kutokana na taarifa ya kuwepo
kwa ugonjwa huu katika nchi jirani ya Kenya, Angola na DRC.
Kwa mujibu wa taarifa ya Shirika la Afya Duniani
hadi kufikia mwezi Oktoba, 2016 tokea mlipuko ulipoanza mwezi Desemba, 2015 imeripotiwa
kuwa idadi ya wagonjwa wa homa ya manjano katika nchi ya Angola ni takribani watu
4,347 na zaidi ya watu 377 walipoteza maisha. Hali kadhalika, katika nchi ya Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo idadi ya wagonjwa ilikuwa 2,987 na zaidi ya watu 121 walipoteza
maisha. Takwimu hizi zinaonesha jinsi gani ugonjwa huu ulivyokuwa hatari na
jinsi unavyoweza kusambaa kwenye nchi zingine. Habari njema, Tanzania haijawahi
kuripoti kuwa na mgonjwa wa Homa ya Manjano toka mwaka 1960.
Ndugu Wananchi,
Kila mtu yupo kwenye hatari ya kuambukizwa ugonjwa wa
Homa ya Manjano, ila makundi yafuatayo yapo katika hatari zaidi ya kupata
ugonjwa huu;
·
Wasafiri
ambao hawajapata chanjo na wanaotembelea nchi ambazo tayari zina maambukizi ya
ugonjwa wa Homa ya Manjano.
·
Watu
wanaojihusisha na shughuli za uwindaji, utalii n,k.
·
Wafanyakazi
wa Viwanja vya Ndege, Bandari na mipaka ya nchi kavu.
Wizara yangu inaratibu utoaji wa Chanjo ya Homa ya Manjano kupitia vituo vilivyoidhinishwa hapa
nchini kwa mujibu wa Kanuni za Afya za Kimataifa, 2005 na Sheria ya Afya ya
Jamii, 2009. Mtu anapopata chanjo hii hupewa cheti maalumu cha chanjo ya Homa
ya Manjano yaani ‘International
Certificate of Vaccination and Prophylaxis’ kama utambulisho kwamba, tayari
amepata chanjo ya Homa ya Manjano.
Hata hivyo, Utoaji wa Chanjo hiyo umekuwa ukikabiliwa na
changamoto ya kuwepo kwa baadhi ya wananchi wasiokuwa waaminifu maarufu kama
‘vishoka’ ambao wanagushi vyeti vya chanjo na kuwapatia wasafiri pasipo
kuchanja. Taarifa za kugushi vyeti ziliripotiwa hata na gazeti la ‘The Citizen’ la tarehe 7 Juni, 2016 na
vyombo vingine vya habari ambavyo vilibainisha uwepo wa vishoka hao nje ya
hospitali ya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam ambao huwalaghai wasafiri na kuwauzia
vyeti pasipo kupewa chanjo. Hii ni kinyume na Sheria ya Afya Jamii ya Mwaka, 2009.
Ndugu Wananchi,
Kutokana na mabadiliko ya teknolojia, vyeti vya zamani
vimekuwa rahisi kutengenezwa na watu na kutolewa bila kupata chanjo, Hivyo Wizara
imefanya maboresho ya vyeti vya chanjo ya Homa ya Manjano kwa kuweka alama za
siri na kutengeneza mihuri mipya. Vyeti hivi sasa vina kurasa 16, (vya zamani
vina kurasa 8) namba ya utambulisho (serial number) na vinatolewa na vituo vilivyoidhinishwa
na Wizara. Aidha vyeti hivi vitaendana na kuweka namba ya utambulisho wa chanjo
(Batch number) iliyotolewa ili kuepusha tabia ya watumishi wasiokuwa waaminifu
kuvitoa bila kuchanja. Vyeti hivi nitavizindua hivi punde.
Ndugu Wananchi,
Ubadilishaji wa vyeti vya chanjo utafanyika katika awamu
mbili kama ifuatavyo;
Awamu
ya kwanza; ilihusisha utoaji wa
vyeti vipya kwa wanaochanja kuanzia tarehe 1 Agosti, 2016 na kuendelea. Gharama
za Huduma za Chanjo ya Homa ya Manjano ni shilingi elfu 20 za Kitanzania kwa
raia wa Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki, kwa raia wa Kigeni ni Dola 50
za Kimarekani.
Awamu
ya pili; itajumuisha ubadilishaji
wa vyeti vya zamani kwa wale ambao walipatiwa chanjo na kupewa vyeti halali vya
zamani. Wahusika wa kundi hili watawasilisha vyeti vya vya zamani kwa Mganga Mkuu
wa Mkoa/Wilaya wa sehemu waliyopo ambaye atawasilisha taarifa zao Wizarani
ambapo zitahakikiwa na wale wanaostahili watatumiwa vyeti vyao mahali walipo. Zoezi hili litadumu kwa takribani miezi
mitatu kuanzia tarehe 09 Januari, 2017 mpaka Machi 31, 2017. Napenda kuwajulisha
kuwa kuanzia tarehe 01 Aprili, 2017 vyeti vya zamani havitatambulika tena.
Ndugu Wananchi,
Ninawaagiza Maafisa Wafawidhi wa Vituo vilivyoidhinishwa na Wizara
kwa ajili ya kutoa Chanjo ya Homa ya Manjano kuzingatia yafuatayo;
1. Kuhakikisha vyeti vya chanjo vinatolewa mara baada ya mtu
kukamilisha malipo na kupewa chanjo na si vinginevyo. Wizara itawachukulia hatua wale wote watakaotoa
vyeti bila kutoa chanjo.
2. Kuhakikisha chanjo inatolewa pale tu ambapo malipo yamefanyika na
kuna risiti halali ya malipo.
3. Kuzingatia maelekezo ya utunzaji wa fedha, ujazaji sahihi wa vyeti
na utunzaji wa kumbukumbu za waliopata chanjo.
4. Kuwasilisha taarifa za waliopata chanjo na vyeti vya chanjo kila
mwezi Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto.
Ndugu Wananchi,
Napenda kuwafahamisha kuwa ugonjwa wa Homa ya Manjano bado
haujaingia nchini. Hivyo, ninawasihi wananchi wote na wasafiri tushirikiane
katika kudhibiti ugonjwa huu usiingie nchini mwetu kwa kuzingatia yafuatayo:-
1. Kuepuka kupokea au kununua vyeti bila kupata chanjo kwani kufanya
hivyo kunahatarisha maisha yako na ya watu wengine. Aidha, toa taarifa kwenye
ofisi yoyote ya serikali iliyo karibu au vyombo vya dola juu ya Afisa au mtu
anayetoa cheti bila kutoa chanjo au mtu anayetoa chanjo bila kutoa risiti.
2. Iwapo unasafiri, kuhakikisha
unapata chanjo siku 10 kabla ya kusafiri na kisha kupewa
cheti cha kuthibitisha kupata chanjo hiyo pamoja na stakabadhi ya Serikali
baada ya kukamilisha malipo. Ifahamike kuwa chanjo ya Homa ya Manjano inatolewa
katika vituo vifuatavyo;
a.
Viwanja vya Ndege
Uwanja wa Ndege wa Kimaitaifa wa Julius Nyerere, Uwanja wa Ndege
wa Kimataifa wa Kilimanjaro na Uwanja wa Ndege wa Mwanza.
b.
Bandarini
Bandari ya Dar es Salaam, Bandari ya Tanga, Bandari ya Mwanza, na
Bandari ya Kigoma.
c.
Mipaka ya nchi kavu
Horohoro, Namanga, Holili, Tarakea, Sirari, Isaka, Mutukula,
Mtambaswala, Kasumulu na Tunduma.
d.
Dar e s salaam
Kituo cha Afya cha Mnazi Mmoja.
3. Wizara inatoa onyo kwa vituo vinavyotoa chanjo bila kuwa na kibali
kuacha mara moja. Hali kadhalika wale wanaochapisha, kusambaza na kuuza vyeti
hivi waache mara moja kwani hatua kali itachukuliwa dhidi yao.
Hitimisho:
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,
Wazee na Watoto inapenda kusisitiza kuwa wananchi wanapaswa kuendelea kuchukua
tahadhari ya Ugonjwa wa Homa ya Manjano hususani wale waliopo katika mikoa
ambayo inapakana na nchi ya Uganda, Kenya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
pamoja na maeneo yote ambayo watu hupita kuingia nchini kwenye mipaka ya nchi
kavu, maziwa, viwanja vya ndege na bandari. Ninawashukuru na ninawaomba tusaidiane katika
kuimarisha udhibiti wa Ugonjwa huu usiingie hapa nchini. Mwisho, napenda
kuchukua nafasi hii kuwashukuru Shirika la Afya Duniani (WHO) na Wadau wengine
wa Maendeleo kwa jitihada zao za kuboresha udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza
yenye hatari ya kusambaa Kimataifa. Asanteni sana.
Baada ya kusema hayo natangaza rasmi kuwa vyeti vipya vya Chanjo
ya Homa ya Manjano yaani International Certificate of Vaccination and
Prophlaxis ambavyo vinatolewa kwa mujibu wa Kanuni za Afya za
Kimataifa, 2005 na Sheria ya Afya ya Jamii, 2009 vimezinduliwa rasmi.
ASANTENI SANA KWA
KUNISIKILIZA.
|
TAARIFA YA MHE. UMMY
MWALIMU (MB); WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO
KWENYE UZINDUZI WA VYETI NA MIHURI MIPYA YA CHANJO YA UGONJWA WA HOMA YA
MANJANO 24 Novemba, 2016