Kuhusu uongozi mpya wa wilaya ya CHADEMA Ubungo
Katibu wa CHADEMA Wilaya ya
Ubungo, Goodluck Justine (wa kanza kushoto) akiongea na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam
|
UONGOZI mpya wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo wilaya ya kichama
Ubungo unatarajiwa kujulikana Agosti 3, 2014 baada ya uchaguzi wa ngazi
za chini katika wilaya hiyo kukamilika.
Mbali na viongozi wa wilaya hiyo kujulikana siku hiyo, pia chama hicho
kimeeleza kuwa, kimejiandaa vema kuwadhibiti mamluki wasijipenyeze
katika uongozi huo.
Hayo yalibainishwa na Katibu wa CHADEMA Wilaya ya Ubungo, Goodluck
Justine, wakati akielezea mafanikio yaliyopatikana katika uchaguzi wa
ngazi za msingi, matawi na kata.
Nafasi zitakazowaniwa ni ya mwenyekiti, katibu, katibu mwenezi na
mhazini na kwamba, kwa ngazi ya mabaraza ni vijana, wazee na wanawake.
Justine alisema, ni fursa kwa kila mwanachama muadilifu wa CHADEMA Wilaya ya CHADEMA Ubungo kuwania nafasi anayoona ataimudu.
Aliwataka wagombea wote wa nafasi mbalimbali za uongozi katika jimbo
hilo kuchukua fomu, kuanzia jana katika ofisi za jimbo ili kuwania
nafasi hizo kwa ngazi ya kichama na mabaraza na siku ya kurudhisha fomu
za wagombea ni Agosti Mosi, mwaka huu saa kumi alasiri.
0 comments:
Post a Comment