Maonesho ya WajasiriaMali Mtwara
Maonesho ya bidhaa mbalimbali za wajasiria mali kutoka pande mbalimbali
za nchi na nchi jirani yamenza mjini Mtwara. Maonesho hayo
yaliyoandaliwa na SIDO na wadau wenzi, yanalenga kuonesha bidhaa anuwai
zitengenezwazo na wabunifu na pia kutafuta masoko toka kwa wadau. Mkoa
wa Mtwara, ambao umesikika masikioni mwa wadau wengi hivi karibu
kufuatia kugunduliwa kwa gesi asilia, unaanza kuwa moja ya masoko
makubwa tarajiwa ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Maonesho haya ambayo yamefunguliwa rasmi na ndugu mwenye dhamana ya viwanda vya Tanzania, ni fursa nzuri ya kuweza kuonesha bidhaa na mwanzo mzuri ya viwanda vyetu wenyewe kuanzia hatua za mwanzo kabisa. Kupitia wadau hawa wa bidhaa hizo ndogo, Taifa linaweza siku za usoni, kama tutaweka mkazo wa kutosha, kuwa na viwanda vyake lenyewe. Ili tuweze kufikia ndoto na lengo hilo ni muhimu kutengeneza mazingira ya kuwawezesha wajarisiliamali wetu kutengeneza bidhaa zao kwa gharama nafuu. Gharama za uzalishaji ikiwa ni pamoja na mali ghafi zikiwa na bei ya chini, itawezesha wadau wengi kujiajiri na bidhaa zao zitakuwa na bei ya chini.
Nasema hivyo kwa kuwa baadhi ya bidhaa nilizoziona zinauzwa kwa bei
kumbwa mno ukilinganisha na ubora wake. Bidhaa nyingi ni za asili
kabisa na hivyo kuwa imara ukilinganisha na zitangenezwazo na makanjanja
mjini, japokuwa ubora wake unahitaji kuongezwa zaidi ili zivutie
wanunuzi wengi zaidi. Nilipohoji juu ya bei mmoja wabunifu wa bidhaa
alisema: "nalazimika kuuza kwa bei ya juu kwa sababu nalipia kodi na
ushuru mbalimbali na pia kwa kuwa hakuna watazamaji wengi nauza bei ya
juu ili kupitia mauzo haya nijikimu hapa mjini". Baadhi ya wadau hawa wa
bidhaa asilia waliomba waandalizi wa maonesho haya wafikilie kuwalipia
baadhi ya gharama ili kumudu vyema zaidi maonesho hayo. (Mwandishi
hakupata fursa kuongea na timu ya maandalizi juu ya suala hili)
Wakazi wa mjini Mtwara, hawajahamasika vya kutosha kutembelea
maonesho hayo, jambo ambalo lingewezesha wajasiriamali kuuza bidhaa zao
na kumudu kujikimu kupitia mauzo hayo. Hata hivyo ni fursa kwa wenyeji
wa mkoa huo kujifunza mbinu mbalimbali za kukabiliana na maisha na
utawala wa mazingira ya binadamu.
0 comments:
Post a Comment