TRAMEPRO
ni Shirika la Dawa Asilia na Ulinzi wa Mazingira (Traditional Medicine and
Environmental Protection Organization) lililosajiliwa chini ya Sheria ya
Mashirika yasiyokuwa ya Kiserikali yaani Non – Govermental Organization (NGO’s)
“Act 24 of 2002” lenye namba ya usajili 00NGO/00007772 linalofanya kazi kwa
Karibu na Serikali na Jamii katika kufuatilia Matumizi sahihi ya dawa asilia ,
uandaaji wa dawa asilia, upatikanaji wa dawa asilia na uvunaji endelevu utakao
pelekea kukua kwa pato la mtu mmoja mmoja na uchumi wa nchi pamoja na kulinda
Mazingira ili kupata dawa asili iliyo na Virutubisho vya kutosha . Uvunaji
makini wa Miti dawa utatuletea upatikanaji wa mvua za kutosha zitakazo
tuwezesha katika kilimo, hewa safi, chakula pia kulinda na kuendeleza BAONUAI.
Dira ni kuwa na Jamii
yenye kuheshimu, kutumia na kulinda Dawa za Asilia zinazotoka katika mazingira
Asili na yaliyolindwa, ili kutuwezesha kuwa na Afya bora, kupambana na adui
maradhi nakutambua vyanzo vinavyoweza kuchafua matumizi yetu Salama na kulinda
usalama wa watumiaji.
Kwapamoja tunawajibu
mbalimbali katika kuangalia upatikanaji na upandaji wa miti dawa ili kupata
dawa kwa wingi na kuendelea kulinda Afya zetu na kutunza mazingira yetu. TRAMEPRO
tunafanya juhudi mbalimbali za kuhakikisha jamii inapata elimu ya matumizi ya
dawa asili na faida zinazopatikana kwa kulinda mazingira yetu .Ili kufanikisha
matumizi sahihi ya Dawa asilia na kulinda Mazingira ni muhimu Kutoa Elimu na
kuwajengea uwezo waganga, watabibu, wavunaji, wakulima, wazalishaji, wauzaji na
Watumiaji wa dawa asilia.
TRAMEPRO kupitia
semina, midaharo, makongamano mbalimbali tuliyoandaa na kushirikishwa
(kushiriki), vipindi katika redio na television pamoja na mitandao yetu ya
kijamii tumejitahidi kuelimisha matumizi sahihi ya dawa asilia na utoaji wa
huduma sahihi za tiba asilia kwa matabibu kwa kufuata sheria, kanuni, taratibu
na miongozo iliyowekwa ili kuhakikisha kuwa jamii inakuwa na uelewa mkubwa juu
ya matumizi sahihi ya dawa asili na kulinda mazingira yetu.
Kwa kutambua Sera,
Sheria, Kanuni, taratibu na miongozo inayo simamia shughuri zetu za kila siku
na kushirikiana na wadau wa afya na Mazingira hasa katika kufanya utafiti wa Dutu za mimea,wanyama,
madini, ndege na wadudu tutakuza sekta yetu ya Tiba Asilia na Tiba Mbadala.
Leo tumekutana hapa na
wadau mbalimbali wa Afya, Tiba Asilia, Tiba Mbadala na mazingira ili kujadili
maelekezo na utekelezaji wa Maagizo ya Serikali ya tarehe 15 Januari 2016
yaliyotolewa na Mhe. Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto
kwa watabibu wa Tiba Asili na Tiba Mbadala, kubadilishana uzoefu, ujuzi na
maarifa kati yetu na wadu wengine juu ya njia bora na sahihi za kuwahudumia wagonjwa,
ili kupunguza madhara yatokanayo na uzembe, ucheleweshaji na matukio mengine
yanayoweza kusababisha ulemavu na vifo.
Pia kutoa elimu nasaha
juu ya afya ya msingi kwa wateja wao, na kuleta uhusiano mzuri na wakaribu kwa
wote, ikiwa ni pamoja na watabibu wa Tiba Asilia na Tiba Mbadala na jamii yote
tukiwa na matarajio ya kuongeza upeo zaidi.
Shirika la dawa Asilia
na Ulinzi wa Mazingira TRAMEPRO linaungana katika Mkutano huu ikiwa ni moja
kati ya mikutano iliyoshiriki na kuandaa ili kupata maoni ya wadau na kuongeza upeo zaidi juu ya huduma za Afya
zinazotolewa kwa Tiba Asilia na tiba Mbadala na namna ambavyo mazingira
yanavyoweza kulindwa.
TIBA ASILI NI NINI?
TIBA ASILI ni Jumla ya
maarifa na utendaji ambao unatumika katika kuchunguza, kukinga na kuponya
ugonjwa wa kimwili, kiakili au kimahusiano ambao unategemea uzoefu wa
kurithishwa toka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo.
TIBA MBADALA NI NINI?
TIBA MBADALA ni Jumla
ya maarifa na utendaji unaotumika katika uchunguzi, ukingaji na uponyaji wa
matatizo ya kimwili, kiakili na kijamii na kutegemea tu mifumo mbalimbali
iliyoanzishwa na Tiba Mbadala ya Nyanja husika.
Huduma hizi zitolewazo
na watu waaina mbalimbali kwa kutumia nyenzo, ujuzi na uzoefu wa kiasili. Tiba
asilia hutofautiana toka jamii au kabila moja hadi jingine. Baadhi ya dawa au
Tiba toka jamii zingine zina ubora wa kipekee kiasi cha kuleta mvuto sehemu
zingine.
MAZINGIRA NI NINI?
Mazingira ni vitu
vyote vinavyotuzunguka vyenye uhai na visivyo na uhai. Vitu vyenye uhai ni
pamoja na mimea na wanyama na visivyo ni pamoja na uhai ni hewa, ardhi na maji.
Mazingira yanahusisha pia vitu vyote vinavyosaidia kuendelea kuwepo kwa maisha ya mwanadamu na viumbe wengine. Hivyo basi maisha ya viumbe hai wa kizazi kilichopo na kijacho kinategemea uwepo wa mausiano mazuri kati ya watu na mazingira.
KAZI ZA MTABIBU WA TIBA
ZA ASILI
Mtabibu wa tiba asili
aliyepata mafunzo anatarajiwa kufanya yafuatayo:-
·
Kutunza kumbukumbu za wagonjwa kwa
utaratibu unaokubalika.
·
Kutambua na kuhamasisha wagonjwa wenye
vidokezo vya hatari na wanaohitaji
rufaa za mapema ili waende kwenye kituo cha afya husika kwa huduma ya utaaramu
zaidi.
·
Kutoa huduma salama kwa kujari afya ya
mgonjwa huku wakiwa wasafi.
·
Kutoa huduma katika mazingira ya usafi.
·
Kutoa elimu na nasaha kuhusu usafi, lishe bora
na utunzaji wa mazingira.
• Kutoa dawa kwa
utaratibu unaokubalika
• Kutunza vifaa vya
huduma na dawa kwa utaratibu unaokubalika
• Kushirikiana na
kuwaelewa watumishi wa afya
• Kupata mwanga juu ya
misingi ya utafiti wa madawa ya asili.
• Kushirikiana na
mashirika, vikundi vyama mbalimbali hususani vya kitaaluma.
• Kupambanua Watabibu
wa kweli na tapeli
• Kutoa ushauri juu ya
kupunguza kasi ya kuenea kwa magonjwa hususani magonjwa sugu kama kansa,
kisukari, magonjwa ya zinaa na Ukimwi
• Kuzingatia sera,
miongozo ya Serikali, sheria na kanuni na taratibu
za kitaaluma.
NAPENDA KUSISITIZA
YAFUATAYO
(i) watoa huduma wa
tiba asili – wachane na upingaji wa ramri zinazogonganisha/Kuchonganisha jamii
na kukosesha amani ndani ya jamii.
(ii) Watoe tiba iliyo
na tija kwa jamii ili tuweze kuokoa maisha ya
binadamu kwani watabibu
wa tiba asilia mlishapewa karama na mwenyezi
Mungu kuokoa maisha ya
watu, hivyo tutowe huduma itakayoendeleza Tiba asilia
(iii) Watabibu wa tiba
asilia tunaitaji kuongeza elimu na bidii za utafiti wa madawa kwa ajili ya
kutibu magonjwa mbalimbali yaliyoshindikana kutibiwa katika jamii zetu.
(iv)Pia wananchi
tunaomba nasi tuachane na dhana potofu kwani nasi pia ni chanzo kikubwa cha
kuleta ugomvi kwa sababu unavyokwenda
kwa mganga kutibiwa kuna tabia ya kulazimisha waganga wawambie wachawi wenu
badala ya kuomba upatiwa dawa stahiki ya kutibu tatizo ulilonalo unayotokana na
mimea asilia.
USAFI NA MAZINGIRA
(I) Mtoa huduma wa tiba
asili anahitajika kwanza mwenyewe awe msafi wa mwili mzima kabla ya kuanza kazi,
nguo zake za kazi ziwe safi, na mazingira yake yawe safi na salama kwa kutolea
huduma ya tiba asilia.
Wagonjwa walazwe mahala
pasafi, vyombo vya kuifadhia madawa na mahala pa kutunzia madawa pawe pasafi,
vifaa viwe safi na salama. Pia anapo fanyia kazi pawe safi, vyoo viwili vyote
viwe safi mabafu yote mawili yawe safi, hadi mavazi ya mganga mwenyewe yawe
safi.
MADHARA YA UCHAFU
Unapokuwa unatoa huduma
ukiwa mchafu basi unaweza kumuongezea mgonjwa wako magonjwa mengine, kumsababishia
magonjwa ya kipindupindu, pumu, vikoozi vya kila wakati, ukimwi, pepopunda,
funza, upele, ukurutu, kichocho na Ukimwi hatimaye kusababisha vifo vya watu.
WATABIBU TAPELI
Wapo watu wasiokuwa na
uelewa juu ya Utoaji huduma ya tiba Aislia wanaodandia na kuchafua jina la
taaluma ya tiba asilia ya kitanzania, wapo watu wasiokuwa na taaluma ya tiba
asili au wanautambuzi mdogo sana kwa taaluma hii. Wapo wasioijua hii taaluma
kazi yao ni kununua dawa kutoka kwa wataaluma, baadaye kujifanya kuwa wenyewe
ndiyo wataaluma zaidi.
• Watu hao ni wasemaji
sana.
• Hujipa sifa wenyewe
• Hujigamba sana
• Hujikweza
• Husema wana weza kutibu
na kuponyesha kila aina ya ugonjwa.
• Ni wadanganyifu mno.
Hizo ni baadhi tu ya
dalili za kutambua matapeli na wao wanajipenda sana zaidi ya mganga mwenyewe na
gharama zao ni kubwa zaidi.
MAADILI YA TIBA ASILI
Watoa huduma za tiba
asilia wanahitaji kuzingatia maadili ya dawa, kazi zao.
(i) Unahitaji kuelewa sera
na sheria za 23/2002 ya tiba asili na tiba
mbadala Tanzania.
(ii) Kutunza siri za
wateja wako
(iv)Kutokuwa na uongo
na udanganyifu.
(v) Kutoendesha
shughuli zako kiutapeli
(vi) Kutolewa wakati wa
kutoa huduma.
(vii) Kutokubaliana na
mteja kulipiza visasi
(viii) Kutopiga ramri
za kuchonganisha
(ix) Kutonyanyasa
wateja wako na kuwapiga,
(x) Timiza hivyo
vipengele utaheshimika sana ndani ya jamii unamoishi.
FAIDA YA DAWA ZA ASILI
1. Inatibu na kuondoa
magonjwa sugu
2. Inastawisha afya ya
binadam zaidi
4. Ina boresha mwili wa
binadam zaidi na ina virutubisho vingi.
Ndugu wananchi tunaomba
tuzingatie utamaduni wetu na mila na desturi nzuri tusibaki kuthamini sana mila
za kigeni Wananchi tugeuze akili zetu tutumie zaidi dawa zetu za asili ili
tuweze kupunguza vifo vingi hapa nchini. Pia tule vyakula vya asili, mfano
vyakula vyote vya nafaka na mafuta ya asili, mtaona mabadiliko ya nchi yenu
kuwa makubwa kwa afya za binadam hata vifo vitapungua hapa nchini.
Mnaona magonjwa
yanazidi kila kunapokucha na tiba hazipo zimebakia za wasiwasi. Nimatumaini
kuwa wananchi watabadili fikira zao ili waokowe maisha yao.
Ahsante
IMETAYARISHWA NA KAMATI
TENDAJI YA TRAMEPRO
CHINI YA KATIBU MKUU
……………………………
BONIVENTURA F. MWALONGO
KATIBU MKUU